Powered By Blogger

Ijumaa, 2 Mei 2014

Makamu wa Askofu asisitiza Katiba bora

MAKAMU wa Askofu Jimbo la Mashariki Kaskazini, Mchungaji Spear Mwaipopo, amesema Kanisa litaendelea kuliombea Taifa na viongozi wake, lakini akawataka viongozi wa nchi hii nao watimize wajibu wao kwa kutenda haki.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam katika ibada ya kuadhimisha miaka 75 ya Kanisa hilo nchini.

Mchungaji Mwaipopo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alisema; "Kama kanisa tutaendelea kuliombea Taifa, lakini na Viongozi wa nchi hawana budi kutimiza wajibu wao wa kulitendea haki Taifa letu kwa kudumisha Muungano, amani na mshikamano na kutupatia Katiba bora inayotokana na maoni ya wananchi."

"Sasa hivi kuna mabishano ya kiitikadi yanayoendelea na sisi tusingependa kuwa na Katiba ya Chama bali ya Watanzania wote... hakuna chama chenye watu zaidi ya milioni 45. Tukiruhusu hali hii tutakuwa hatuwatendei haki Watanzania walio wengi," alisema.

Alisema kila jambo jema hushuka kutoka kwa Baba wa mianga na kwamba kama Kanisa wamekuwa wakiliombea jambo hilo, hivyo anaamini kwamba Mungu atalisimamia hadi mwisho.

Aliwataka waumini wa Kanisa hilo kuendelea kuomba bila kuchoka. "Kwa hiyo wapendwa msiangalie malumbano tu ndani ya TV, bali endeleeni kuomba ili jambo hili aliloliazimia Bw. Liweze kutimia," alisema.

Alisema anafurahishwa na ukweli kwamba Kanisa la TAG linaadhimisha miaka 75 wakati Taifa la Tanzania limetimiza miaka 50 hapo jana tu (Aprili 26, 2014).

"Nawapongeza Marais wetu wastaafu hayati Mwl. Nyerere na Abeid Amani Karume kwa kudumisha Muungano wetu na kuruhusu kikatiba uhuru wa wananchi kuabudu. Kudumu kwa Muungano kumetusaidia kuweza kuhubiri Injili hadi Zanzibar," alisema.

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG-Taifa) lilianzishwa mwaka 1939 na kanisa la kwanza hapa nchini lilijengwa katika kijiji cha Igale, mkoani Mbeya.

Jumanne, 22 Aprili 2014

666 CHRISTIAN BONGO MOVIE UNYAKUO PALAPANDA

FILAMU YA KIKRISTO KUHUSU SIKU ZA MWISHO,
IMEANDALIWA NA REV. JOSHUA KADUMA.

Ijumaa, 18 Aprili 2014

TAZAMA VIDEO MPYA YA JOYOUS INAYOZINDULIWA RASMI LEO



Angalia moja kati ya nyimbo mpya katika toleo la 18 la Joyous Celebration uitwao Bhekani uJehova, wimbo ambao awali kabla kanda haijaanza kuuzwa ulikuwa ukitolewa kama zawadi kwa wanunuzi wa nyimbo za kundi hilo kupitia album hiyo mpya katika mtandao wa iTune. Joyous inaanza rasmi uzinduzi wa ziara zao kwa mwaka huu kupitia album hiyo iliyopewa jina la 'One purpose' katika ukumbi wa Carnival City jijini Johannesburg nchini Afrika ya kusini. Natumaini utabarikiwa, uwe na ijumaa kuu njema yenye kuleta maana halisi katika maisha tuyaishiyo nasio kwa kuzungumza. Barikiwa




PATA MKUSANYIKO WA NYIMBO ZA KUKUMBUKA MATESO YA YESU


Mdau wa GK leo tumekuwekea baadhi ya nyimbo ambazo hapana shaka zitakubariki moyo wako katika siku hii maalumu ya kukumbuka mateso na kifo cha mkombozi wa ulimwengu Yesu Kristo.

Anza na wana Kijitonyama Uinjilisti kwaya na wimbo uitwao 'Nakimbilia Msalabani' wimbo huu ulirekodiwa wakiimba katika moja ya ibada kanisani kwao Kijitonyama Lutheran (Si rasmi, bali mtu alirekodi kwa matumizi yake) hapana shaka utabarikiwa nao.



Hapa tunao wana AIC Chang'ombe Choir (CVC) katika album yao iliyopita iitwayo Jihadhari na Mpinga Kristo' wimbo tumekuchagulia 'Inasikitisha sana'.

Tunaye Flora Mbasha katika moja ya nyimbo ambazo mpaka leo zinabariki na kugusa wengi licha ya kwamba aliimba miaka takribani sita iliyopita. Wimbo unaitwa 'Aliteseka'

Hapa tunao kwaya iliyotamba sana miaka ya mwanzo ya 90 jijini Dar es salaam, ikifahamika kwa jina la kwaya mtakatifu Maurus kanisa Katoliki Kurasini. Kutoka kwao tumekuchagulia wimbo Yesu Akalia.
 

Mitaa ya Kinondoni, jijini Dar es salaam, tunakutana na kwaya ya Kinondoni kanisa la Kisabato, kwaya ambayo ilivuma sana enzi zake chini ya mwalimu wao Gideon Kasozi, kutoka kwaya hii tumekuchagulia wimbo 'Yesu Alisononeka'.



Malizia na wana Kinondoni Revival kutoka Assemblies of God, kwaya ambayo imeendelea kusimama katika utumishi kwa miaka kadhaa na kuendelea kubariki wengi. Kupitia album yao ya Mtu wa nne ambayo bado haijapata mrithi wake, tumekuchagulia wimbo uitwao 'Imekwisha'. Tunakutakia Ijumaa Kuu yenye tafakari kuu juu ya maisha yako na yangu.

TAMBUA NGUVU YA MUNGU ILIYOPO KATIKA KINYWA CHAKO.




BWANA YESU asifiwe Wana wa MUNGU.
Napenda kuleta kwenu somo hili:

                        Je Unakiri nini?

 “Nanyi mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu ROHO MTAKATIFU, (Matendo 1: 8).
Je, tunatumia hii nguvu ya MUNGU?
Na je tunaitumia  mamlaka ya KRISTO tuliyopewa kama inavyotakiwa?
Haijalishi mwana wa MUNGU unapita katika magumu kiasi gani, Unachotakiwa ni kubadilisha kukiri kwako, na kadri unavyotamka kinyume na mazingira yanavyoonekana,elewa kuna jambo katika ulimwengu wa Roho linafanyika, hata kama huna shilingi mia mfukoni wewe sema pesa zipo,  hata kama wewe ni mgonjwa umelala kitandani Sema mimi ni mzima, maana Neno la MUNGU  linasema aliye dhaifu na aseme ana nguvu.
 Ezekieli alipoonyeshwa lile bonde la mifupa mikavu, kwa macho  ya damu na nyama aliona haiwezekani kwa ile mifupa mikavu kuwa na uhai tena ,lakini MUNGU akamwambia itabirie hii mifupa mikavu ipate kuishi.
Ndipo Ezekieli akatambua nguvu iliyopo katika kinywa chake, akaanza kutoa unabii na kuitabiria ile mifupa, akaiambia  ’’ enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la BWANA; BWANA MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi .Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, nakutia pumzi ndani yenu nanyi mtaishi.’’  Maneno haya tunayapata katika kitabu cha (Ezekieli 37:1…..)
Katika maandiko haya tumeona, ni jinsi gani Ezekiel ialivyoweza kutumia nguvu na uweza ulioko ndani ya kinywa chake na kuweza kuleta uhai tena. Na wewe mwana wa MUNGU nini ni kimekuwa mifupa mikavu katika maisha yako?
-Yamkini ni ndoa ndio imekuwa mifupa mikavu itabirie nayo itakuwa hai tena,
-au ni uchumi wako,
- afya yako,
-watoto wako,
-hudumayako,
MUNGU anakuambia leo simama na uvitabirie, maana kuna nguvu katika kutamka.


Unakiri nini kushindwa au kushinda?
Nguvu ya MUNGU iko juu yako, badilisha yale yote yanayoonekana kuwa yameshindikana na yatawezekana kupitia kinywa chako katika Jina la YESU KRISTO mwenye nguvu zote. AMEEEN.
MUNGU awabariki sana.  
HEZRON MARWA MWANAFUNZI WA YESU
Cell: 0767674089

Jumamosi, 12 Aprili 2014

ALEX MSAMA WA MSAMA PROMOTION APATA AJALI DODOMA HAPO JANA

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amepata ajali baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka wakati akielekea mkoani Dodoma.Chazo cha ajali

kilitokana na yeye kumgonga kijana aliyekua akiendesha basikeli na matokeo yake gari aliyokua akiendesha kupinduka mara 3.Kwa sasa Msama anapatiwa matibabu katika hospitali moja mjini Dodoma.
Picha zote kutoka kwenye Istagram ya mchekeshaji Steve Nyerere
                            Alex msama akiwa hospitalini baada ya ajali.Kulia ni mwenyekiti wa bongo movie Steve Nyerere  
                 

ALEX MSAMA WA MSAMA PROMOTION APATA AJALI DODOMA HAPO JANA

ALEX MSAMA WA MSAMA PROMOTION APATA AJALI DODOMA LEO

Jumatano, 9 Aprili 2014

NAMNA YA KUOMBA

- Hatua na vipengele muhimu katika kuomba -

MKARIBISHE ROHO MTAKATIFU. *Rum 8:26-27 *Yoh 14:16-17
Yesu alisema Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu. Atatusaidia na kutufundisha yote, kwa maana pasipo yeye, sisi hatuwezi neno lolote. Na sisi peke yetu hatujui kuomba ipasavyo, bali yeye (Roho) ajua kutuombea kwa Mungu kama vile Mungu apendavyo. Hivyo kabla ya kuanza maombi au kusoma neno au ibada au safari au mitihani au kikao n.k. jifunze kujikabidhi kwa Roho Mtakatifu, uombe msaada wake, akupe ufanisi/ubora katika yote yakupasayo kufanya.
Tambua Utu wake, Uungu na Uweza wake.
Jikabidhi katika Nguvu ya Uongozi wake.
Tii kila Uongozi anaokupa.
FANYA TOBA NA UTAKASO. *Isa 59:1-2, Yoh 9:31, 1Yoh 1:8-9,7
Sikio la Bwana si zito kusikia wala mkono wake si mfupi kushindwa kututendea mambo tumwombayo, bali maovu yetu ndiyo yanatufarakanisha na Mungu wetu. Mungu hawasikii wenye dhambi. Hivyo chukua muda wa kutafakari na kuungama dhambi zako mbele za Mungu na kuzitubu kwa kumaanisha kuziacha. Mungu ni mwaminifu kutusamehe na kututakasa na uchafu wote. (Isa 1:18). Lakini, kabla hujafanya toba yako binfsi;
(i) - Kwanza, samehe wote waliokukosea, hata kama hawajaja
kukuomba msamaha. Usipowasamehe waliokukosea, na Mungu
hataweza kukusamehe wewe. (Math 6:12,14-15)
(ii) - Ndipo nawe ufanye toba yako binafsi. Na Mungu atakusamehe kabisa.
Hata kama ni nyekundu sana, zitakuwa nyeupe sana. (Isa 1:18, Isa 43:25)
3. MSIFU, MUABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Zab 147 na Zab 148
Msifu Bwana kwa Matendo yake makuu, mwabudu Bwana kwa uzuri wake na kwa sifa zake. Mwadhimishe Mungu kwa Tabia zake, wema wake, fadhili zake na baraka zake mbalimbali anazotutendea. Sifa yako ikifika vizuri mbele za Mungu, ndipo atakuwa tayari kukupa haja za moyo wako. Haja zetu zimefichwa nyuma ya mgomgo wa sifa. Ndio maana Neno linasema;
‘Nawe utajifurahisha kwa Bwana (kwa kumsifu, kumwabudu na kumshukuru), naye atakupa
haja za moyo wako’ (Zab37:4).
Yesu anatuonyesha mfano; angalia sentensi yake ya kwanza katika kuomba kwake imekuwa “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.” (Math 6:9). Anaanza maombi kwa kumsifu Mungu. Msifu Mungu kwa kuimba na kwa kunena/kusema/kuelezea. Mungu anataka kusifiwa na kutukuzwa. Ukifanya sifa nzuri, ya kuufurahisha moyo wake, atakupa hata na vile ambavyo hukutegemea/hukuomba.
4. MWELEZE MUNGU MAHITAJI NA HOJA ZAKO. *Wafilipi 4:6-7,19 Isa 43:26
Mweleze Mungu zile hoja zilizokusukumwa kwenda kumwomba. Nenda mbele za Mungu kama ‘kuhani’ (1Pet 2:9). Kwa unyenyekevu na heshima. Lakini kabla ya kumweleza mahitaji yako binafsi;
(i) Kwanza fanya ‘maombezi’ – ombea watu wengine; (1Tim 2:1-4)
Viongozi mbalimbali na wenye mamlaka, watumishi wa Mungu, marafiki zako, wenye shida, ndugu zako, nchi yako, shule yako, shirika lenu, ofisi yenu, chama chenu, n.k. Usianze kujiombea mwenyewe tuu, zoea kuwatanguliza wengine.
(ii) Kisha fanya ‘maombi yako’– ombea haja za moyo wako. (Math 7:7-11)
Mweleze Mungu haja zako. Ongea na Mungu kwa uwazi na ukweli. Japo anazijua haja zetu, lakini ameagiza kuwa tumwombe ndipo atafanya. ‘aombaye hupokea’ yaani; asiyeomba, hapati. Mungu anasema tumpelekee hoja zenye nguvu (Isa 41:21). Omba vitu vizuri na mambo makubwa ili upewe (pray for good things and big things)
5. FANYA MAOMBI YA VITA VYA ROHONI. *Efe 6:10-13 *2Kor 10:3-5
Baada ya kumwendea Mungu na kumweleza mahitaji yako, sasa simama kama ‘mfalme’, kwasababu wewe ni ‘mfalme’ (Ufu 5:8), tumia mamlaka yako ya kifalme, ongea na hali/hitaji ulilokuwa unaliombea, na kwa mamlaka, amuru iwe kama vile ulivyoomba/unavyotamani. Ndio maana Bwana Yesu alipokabidhiwa mamlaka yote na Mungu, naye akatukabidhi sisi (kanisa lake) “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui. Wala hakuna kitakachowadhuru” (Luk 10:19, Yer 1:10, Yak 4:7). Tuma neno lenye mamlaka katika hali/jambo ulilokuwa unaliombea, Amuru iwe vile ulivyokuwa unamwomba Mungu iwe. Kemea kila roho ya shetani inayoweza kuwa inasababisha tatizo katika swala lako.
6. OMBEA ULINZI JUU YA ULIYOYAOMBEA. *Math 6:13a
Baada ya kupiga vita vya kiroho, weka ulinzi katika yale uliyoyaombea, ili shetani na mapepo yake wasiweze kuirudia hali/jambo/mtu yule uliyemkomboa kwa maombi ya vita. Yesu alisema shetani akifukuzwa mahali, haendi mbali, anasubiri kuona kama atapata upenyo wa kuparudia mahali pale alipokuwa kwanza. (Math 12:43-45). Kwahiyo, usipoweka ulinzi, kuna uwezekano wa adui kurudi na kuliharibu zaidi lile jambo uliloliombea na kulipata.
Kumbuka, unapoomba vizuri, unapokea papo hapo (katika ulimwengu wa roho), lakini udhihirisho wake katika ulimwengu wa mwili, unaweza kuchukua muda fulani. Hivyo katika muda huo wa kusubiri, shetani anaweza akapita na kuzuia au kuharibu kile unachokisubiri kidhihirike katika ulimwengu wa mwili. Ndio maana Yesu alitufundisha kuombea ulinzi, “tuokoe na yule mwovu” (Math 6:13a). Weka ulinzi juu ya mambo yako yote. Jengea wigo wa moto wa mbinguni (2Fal 6:16-17), Yafunike kwa damu ya Yesu na agiza malaika walinzi walinde mambo yako masaa yote. Omba hivyo kila siku. (Zab 34:7, Zab 91:9-11, Ebr 1:13-14)
MSIFU, MWABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Math 6:13b
Yesu alianza maombi kwa kumsifu Mungu na kumtukuza. Na akamaliza maombi yake kwa kumtukuza Mungu tena. Akasema “kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu ni zako, sasa na hata milele” akamaliza. Kwahiyo nawe kwa kumaliza maombi yako, msifu na kumshukuru Mungu tena, kwa ukuu wake, uaminifu wake, na ahadi zake juu yetu. Ndipo ufunge maombi yako.
MUHIMU: TUMIA MAANDIKO KATIKA KUOMBA *Kol 3:16
-Katika kuomba kwako, mara zote tumia maandiko kumkumbusha Mungu ahadi zake .(Isa 43:26). Mungu analiangalia neno lake ili alitimize. Sababu pekee itakayomfanya Mungu akupe alichoomba, ni ili kulitimiza neno lake. Hivyo, baada ya kumweleza unachohitaji (kwa ajili yako au kwa ajili ya mtu unayemwombea) mpe Mungu andiko/neno lake linalokupa wewe uhalali wa kuomba hicho kitu mbele zake na kupewa.
-Hata unapompinga na kumkemea shetani, baada ya kutoa amri yako dhidi yake, shetani atasubiri kusikia andiko/neno linalomnyima yeye uhalali wa kushika alichoshika. Ndio maana Yesu alimshinda shetani kwa neno la Mungu. Alisema “imeandikwa” na shetani akashindwa. “Nao wakmshinda (shetani) kwa damu ya Yesu na kwa Neno” (Ufu 12:11)
 MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA VIZURI  KWA MUDA MREFU
1. CHAGUA MAHALI PAZURI PA UTULIVU. *Mk 1:35
ili uweze kuomba kwa utulivu na kwa umakini, chagua au tafuta mahali pazuri
patakapokupa utulivu katika kuomba (concentration in prayer). Ndio maana Mungu
alipenda kuongea na Musa juu ya mlima. (Kut 24:12-18). Hata Yesu alizoea kwenda
kuombea mlimani, mahali palipo mbali na vurugu za watu, alipenda kwenda mlimani.
(Math 14:22-23). Tafuta mahali patulivu; chumbani, kanisani, mlimani (Math 6:5-6)
2. CHAGUA MUDA MZURI. *Mhu 3:1,7
Ili uweze kuomba kwa umakini mzuri, chagua muda mzuri ambao akili yako ma mwili
wako viko fresh. Usilazimishe kuomba hata kama akili yako au mwili wako umechoka sana. Kila jambo lina wakati wake. Kama umechoka sana, huo si muda wa kuomba, bali wa kupumzika. Usilazimishe ratiba. ni bora upumzike ili baadaye uweze kuomba vizuri baadaye. Usije ukajikuta unamkemea Yesu badala shetani. Penda kuomba wakati una nguvu ya akili na mwili, ili uwe makini kuongea na Mungu kwa akili timamu. Ndio maana Yesu alipenda kuamka alfajiri sana kwenda kuomba mlimani. (Mk 1:35, Luka 4:42)
3. OMBA KATIKA ROHO (NENA KWA LUGHA). *Efe 6:18, Rum 8:26-27
Mbinu nyingine nzuri ya kuomba kwa muda mrefu na kwa ufanisi, ni kuomba kwa Roho; yaani kuomba kwa kunena kwa lugha. Tunapoomba kwa akili za kibinadamu, Mungu anasikia pia, lakini maombi yako yanakuwa na mipaka / limited kwasababu akili ya mtu haijui kila kitu. Bali Roho wa Mungu anajua kila kitu. Naye hutupa kipawa cha kuomba kwa lugha ya mbinguni iliyo bora zaidi. (Yuda 1:20, Mk 16:17, 1Kor 14:1-4, 15-16,7)
4. OMBA KWA KUFUNGA WAKATI MWINGINE. *Math 6:16-18
Kufunga kula kunasaidia kudhoofisha mwili, ili roho iwe makini zaidi kuongea na Mungu kwa kina zaidi. Mwili huu siku zote haupendi kufanya mambo ya Mungu. Na mwili ukiwa umeshiba, unakuwa na uchovu na uzito wa kufanya mambo ya kiroho. Mbinu mojawapo ya kuudhibiti, ni kuunyima/kuupunguzia posho yake ya chakula. Mwili ukidhoofika kiasi, roho yako inapata nguvu na upenyo mzuri zaidi (Zab 35:13). Mashujaa wote wa imani walifunga na kuomba. Ndio maana Yesu anasema ‘mfungapo’ akimaanisha ratiba ya kufunga, ipo. Inasaidia.
5. OMBA NA RAFIKI (PRAYER PARTNER). *Mhu 4:9-10
Neno la Mungu linasema, ni heri wawili kuliko mmoja. Kuna faida ya kuomba pamoja na rafiki yako. Kwanza, mnapokuwa wawili au watatu, inaleta hamasa na ari ya kuomba zaidi. Si rahisi kujisikia mvivu unapokuwa na waombaji wenzako. Pili; nguvu ya kiroho inaongezeka. Neno linasema, mwombaji mmoja anafukuza adui elfu moja, bali wakiwa wawili, wanafukuza (sio elfu mbili) bali elfu kumi! Shangaa! (Kumb 32:20) Hiyo ni kanuni ya mbinguni/kanuni ya Ki-Mungu. Kadri mnavyoongezeka, nguvu ya Mungu huongezeka.
Kwahiyo, wakati mwingine, omba na rafiki yako, unayemwamini, unayeweza kumshirikisha mambo yako ya binafsi. Mashujaa wengi wa imani, walikuwa na marafiki wa kiroho. (Prayer Partners). Kwa Mfano:- Math 17:1-9
Musa - alikuwa na Joshua, Haruni na Huri
Eliya - alikuwa na Elisha
Daniel - alikuwa na Shadrack, Meshack na Abednego.
Yesu - alikuwa na Petro, Yakobo na Yohana.
Paul - alikuwa na Barnaba, Timotheo na Tito.
Wewe Je? Uko na nani katika urafiki wa kiroho?

Kama huna rafiki wa karibu wa kuomba naye, usikurupuke kujichaglia. Tulia umwombe Mungu akupe mtu atakayekuwa wa msaada kwako. Mtu mtakayefungamanishwa naye katika roho, hata kama mmetengana kijiografia, lakini katika roho, mko na umoja mzuri wa imani. (Math 18:18-19)
6. OMBA KATIKA MKAO UNAOKUPA UHURU NA NGUVU ZAIDI.
Katika kuomba kwa muda mrefu, mkao uliouzoea utakusaidia kwenda mwendo mrefu. Yakupasa kujua nguvu yako na udhaifu wako (strong point and weak point). Wakati wa kuomba, epuka mikao inayokuchosha haraka na tumia mikao inayokua nguvu zaidi. Kwa Mfano:- Ukiwa umechoka, usipende kuomba kwa kupiga magoti au kwa kuegemea kitandani. Ni bora uombe ukiwa umesimama au unatembea tembea, ili kuepuka usingizi na uchovu. Waombaji hodari wanaujua mikao inayowasaidia kuomba maombi marefu. Wengine hawana mikao maalum, bali wakiwa katika maombi, huwa wanabadilisha-badilisha mikao ili wasichoke. Hiyo ni mbinu nzuri pia.
Mifano ya Mashujaa wa imani;
Ibrahim – aliomba kwa kusimama (Mwa 18:22)
Daniel - aliomba kwa kupiga magoti (Dan 6:10)
Paul - aliomba kwa kupiga magoti (Efe 3:14)
Yesu - aliomba kwa kulala chini (Math 26:38-39)
Eliya - aliomba kwa kukaa chini na
kuweka kichwa kati ya miguu (1Fal 18:42)
Mimi - huwa napenda kuomba kwa kutembea tembea
Naweza kumaliza kilomita nyingi chumbani kwangu
Nikitembea huku nikiomba.
Wewe Je? Unaujua mkao wa nguvu? Kama hujui, Tafuta kujua.
OMBA NA MUZIKI LAINI KWA KUMWABUDU MUNGU.
Muziki wa kiroho, na wataratibu, unaweza kukutengenezea mazingira mazuri sana ya kuomba kwa muda mrefu. Muziki wa kuabudu, unavuta uwepo wa Mungu kwa namna ya pekee. Neno linasema, waimbaji na wanamuziki walipoimba na muziki ukapigwa, nao wakawa kama mtu mmoja, utukufu wa Mungu ukashuka na kulijaza lile hekalu hata makuhani hawakuweza tena kuhudumu (2Nyak 5:12-14). Kule mbinguni, kila malaika wa sifa, ana kinubi (zeze/gitaa). Elisha hakutoa unabii, mpaka mpiga kinubi alipopiga kwa ustadi, ndipo mkono wa Bwana (Roho wa Mungu) alipokija juu yake, naye akatabiri.
Najaribu kukuonyesha, kuna connection kati ya muziki wa kiroho na utukufu wa Mungu. Kwahiyo, ukiweza kuomba huku umeweka kanda au CD ya nyimbo za kiroho za taratibu, utapata (experience) hamasa ya kiroho (motivation) na utasikia una nguvu ya kuomba kwa muda mrefu. Kama unaweza, tengeneza kanda au CD maalum yenye nyimbo nzuri unazozipenda wewe, ili uwe unaipiga wakati wa maombi. Utajikuta unaweza kuomba kwa muda mrefu na kwa bubujiko zuri zaidi

MAONI KUHUSU BLOG

Bwana Yesu Asifiwe! Ikiwa ungependa kuwasiliana nasi unakaribishwa. Tutashukuru ukitupa ushauri, kutuonya au kusema lolote lenye kuujenga mwili wa Kristo. TU WAMOJA katika KRISTO. Karibuni MZIDI kubarikiwa.

Jumanne, 8 Aprili 2014

Kwa watu wa Mungu!

mwilii

Watu wa Mungu, ashukuriwe Mungu atupaye uzima na ya kwamba tu hai tena kwa neema yake.

Tunalo la kujivunia lakini si katika miili hii tuliyo nayo bali kwa kuwa tumeipata neema ya Jehova.

Ndugu wapendwa imetupasa kuwa na juhudi sana kuzidi sana katika kulijua Neno la Mungu ili tuwe na hakika na ushindi katika hatari nyingi za dunia.

Maana ”dunia” inasema inayo mazuri, lakini si mbele za Mungu, maana ifahamike hivi; yaliyo yote mazuri duniani ni yaliyo mabaya mbele za Mungu na yaliyo mabaya mbele za Mungu ni yaliyo mazuri kwa duniani, basi kila mtu na asema na akili yake mwenyewe.

Kwa hali hiyo basi; sisi tulio kwa Mungu sawa sawa twajua hivi, kheri uongo wa Mungu kuliko ukweli wa dunia, maana ikiwa kwa uongo huo wa Mungu sisi tu hai rohoni tukiiponya miili hii, basi una faida gani ukweli wa dunia ambao kwa huo tumehitirafiana sisi kwa sisi?

Nasema tena ikiwa kwa uongo huo wa Mungu hatukuwa wazinifu, naam hatujawa walawiti, hatujawa waasherati, hatujawa wafiraji, je si zaidi basi ya huo ukweli wa dunia ambao katika huo tu wanafiki?

Mwaonaje ninyi,
Maana si kwamba hatuoni ama hatusomi alama za kuenenda kwetu na kuishi kwetu maana kila mmoja wetu yu barozi na shahidi wa nyendo zake mwenyewe, jifunzeni katika hili.

Sikia yupo mmoja aweza sema amemaliza kwa sababu ya huu tuuitao wokovu lakini asijue ya kwamba yu apaswa kutambua wokovu ni mbegu iishiyo katika tunda bovu ambalo ni mwili wake mwenyewe.

Maana miili ni kikwazo sana katika maisha ya kuuishia haki, maana tumeokoka ndiyo lakini hatujaihama miili hii.

Siku 2 za maombi ya kufunga Maryland, karibu sana!.

maombi..
Ongeza kichwa

Hezron mwanafunzi wa yesu tutakutana pamoja tarehe 21-23 March, 2014 kwenye maombi ya kufunga na kuomba kwa siku mbili. Kuanzia Ijumaa usiku ni mkesha wa toba, Jumamosi ni mafundisho, maombi na maombezi mpaka Jumapili jioni tutafungua kwa pamoja. Kutakuwa na watumishi mbali mbali watakaohudumu siku hizo!

Kwa wale wangependa kuhudhuria maombi haya karibuni sana, na ikiwa una mtu anayehitaji kuombewa usisite kumleta. Ikiwa hutaweza kuhudhuria na ungependa tuombe pamoja tutafurahi kufanya hivyo.

Kiwango cha Mungu – Double Agent

kanisa
UTANGULIZI.
Pamoja na mabadiliko makubwa ya nyakati zetu katika siasa, uchumi utamaduni (maadili) na kidini. Mungu anacho kiwango chake ambacho ndicho anakubaliana nacho katika maisha yetu. Ili tuweze kuishi na kufiti katika mipango na makusudi yake ni lazima tuangalie kukitunza kiwango cha Mungu katika maisha yetu.
“Kwa kuwa mimi Bwana si kigeugeu (sibadiliki)” Malaki 3:6 Biblia inaonyesha kuwa tumeitwa na tumfananie Mungu na kamwe si Mungu atufananie sisi. Kwa hali hiyo kama hali yetu haifanani na Mungu wito ni sisi kubadilika na wala si Mungu abadilike awe kama tunavyotaka sisi au rafiki zetu, mazingira yetu au jamii. Biblia huonyesha kuwa sisi tunabadilishwa toka UTUKUFU hadi UTUKUFU. Mungu anatunza kiwango chake na kiwango cha Mungu kinakwenda sawa sawa na Neno lake.
Biblia huonyesha mtu hufanana na mawazo yake. “Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo…”.Mithali 23:7 (Tafsiri ya King James hutumia kufikiri badala ya kuona katika nafsi.) Neno la Mungu ni mawazo ya Mungu; kwa hiyo linamfunua Mungu vile alivyo. Ili tumfananie Mungu inabidi tulitafakari Neno lake. Ndipo litaumba picha ya ki-Mungu katika mawazo yetu. Wala tusifanye kuifuatisha dunia na kuwaza ya dunia tu.“Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji” Hosea 5:10
Wito wetu ni kutunza kiwango cha Mungu. Sisi ni vielelezo. Kiwango cha Mungu kinamtambulisha Mungu wetu katika jamii kama Jehova Nissi. Yaani yeye ni bendera yetu. Mfano mzuri ni jinsi Musa katika vita dhidi ya Amaleki alivyonyanyua kiwango cha Mungu (fimbo iliyowakilisha mamlaka ya Mungu) na hapo Joshua alishinda vita. Watumishi na viongozi wa kiroho wakinyanyua kiwango hiki ambacho ni neno la Mungu kina Joshua (kanisa) wanashinda vita. Kiwango kikiondolewa kanisa na taifa hupoteza mwelekeo. Kutoka 17: 11-15
DOUBLE AGENT
Kuna watu ambao katika ujasusi( upelelezi) hufanya kazi pande zote mbili huku kila upande ukiamini unafanyiwa kazi wenyewe. Double agent anakubalika pande zote na hulipwa mshahara na pande zote. Na katika ujasusi huyu ndiye mtu wa hatari ambaye akipatikana hawezi kusamehewa. Ndani ya kanisa pia wamo double agents. Kanisa la Laodikia walionywa kuacha tabia hii mbaya.
“Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala moto (wewe ni double agent);” Ufunuo 3:15 Haiwezekani kutunza kiwango cha Mungu kisha ukaonekana kote kote. Lazima uweke msimamo na dira itakayotambulisha matakwa na kiwango cha Mungu.
Ni lazima tufike mahali tunamtambulisha Mungu katika kila hatua ya maisha yetu kwa viwango vyaUPENDOwetu,UAMINIFU, USAFI, UVUMILIVU, UKARIMU, HURUMA, UNYENYEKEVU NA UTII.Sharti ifikie hatua maisha yetu yanaakisi hali ya Mungu wetu. Hapo tunaweza kuwa manabii( wasemaji wa Mungu) kwa kizazi chetu. Watu wanaotuona wapate ujumbe wa jinsi Mungu alivyo na anavyotaka katika maisha yao. Hatuwezi kuridhia maovu na kuchukuliana na udhaifu wa dunia hii na bado tutegemee kuwa nuru. Mungu atusaidie kuwa watu wanaosimamia kiwango cha Mungu katika siku zetu na hapo maisha yetu yatakuwa na faida katika ufalme wa Mungu.

Jumanne, 3 Desemba 2013

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZA MWILI WA MAREHEMU PAUL WALKER WA FAST AND FURIOUS ULIVYOONYESHWA


HII NDIO INTERVIEW YA YULE SHUJAA WA WESTGATE AMBAYE NI KIVUTIO CHA WATU WENGI HIVI SASA


haji 

Kitu kikubwa ambacho watu wengi walikuwa wanajiuliza kuhusu Abdul Haji ni kwamba yeye ni askari au mwanajeshi, kumbe hana hata mafunzo rasmi ya polisi au jeshi. Haji anasema gaidi mmoja anaweza kuwa ni mkenya na alikuwa anaongea kiswahili.
Ukiachana na ushujaa wake wa kujitoa kuwasaidia watu walikuwa ndani ya lile jengo, kitu cha kwanza kilichomvuta kwenda mle ndani ni ndugu yake wa pekee wa kiume alikuwa ndani humo. Lakini alivyofika ndani na ndugu yake kufanikiwa kutoka alipatwa na hasira za kuendelea kuwasaidia wengine.Angalia interview hii na ambayo anasimulia kila kitu

HEZZO Radio Tanzania


  • Your Official Sheng Station, Streaming Live 24/7 From Nairobi, Kenya. Follow us on Facebook and Google+! Twitter @Ghettoradio895



Rate this track votes
Powered by Thisisafr

Jumatatu, 2 Desemba 2013

TAZAMA TWEET YA TYRESE,VIN DIESEL NA LUDACRIS MARA BAADA YA KIFO CHA PAUL WALKER WA FAST AND FURIOUS..!!


Katika hali ya simanzi na maumivu makubwa, hii ndiyo tweet aliyoandika Vin Diesel mara baada ya mshikaji wake na swahiba wake mkubwa Paul Walker kufariki kwa ajali ya Gari iliyotokea jumamosi mchana