Angalia moja kati ya nyimbo mpya katika toleo la 18 la Joyous Celebration uitwao Bhekani uJehova, wimbo ambao awali kabla kanda haijaanza kuuzwa ulikuwa ukitolewa kama zawadi kwa wanunuzi wa nyimbo za kundi hilo kupitia album hiyo mpya katika mtandao wa iTune. Joyous inaanza rasmi uzinduzi wa ziara zao kwa mwaka huu kupitia album hiyo iliyopewa jina la 'One purpose' katika ukumbi wa Carnival City jijini Johannesburg nchini Afrika ya kusini. Natumaini utabarikiwa, uwe na ijumaa kuu njema yenye kuleta maana halisi katika maisha tuyaishiyo nasio kwa kuzungumza. Barikiwa
PATA MKUSANYIKO WA NYIMBO ZA KUKUMBUKA MATESO YA YESU
Mdau wa GK leo tumekuwekea baadhi ya nyimbo ambazo hapana shaka zitakubariki moyo wako katika siku hii maalumu ya kukumbuka mateso na kifo cha mkombozi wa ulimwengu Yesu Kristo.
Anza na wana Kijitonyama Uinjilisti kwaya na wimbo uitwao 'Nakimbilia Msalabani' wimbo huu ulirekodiwa wakiimba katika moja ya ibada kanisani kwao Kijitonyama Lutheran (Si rasmi, bali mtu alirekodi kwa matumizi yake) hapana shaka utabarikiwa nao.
Hapa tunao wana AIC Chang'ombe Choir (CVC) katika album yao iliyopita iitwayo Jihadhari na Mpinga Kristo' wimbo tumekuchagulia 'Inasikitisha sana'.
Tunaye Flora Mbasha katika moja ya nyimbo ambazo mpaka leo zinabariki na kugusa wengi licha ya kwamba aliimba miaka takribani sita iliyopita. Wimbo unaitwa 'Aliteseka'
Hapa tunao kwaya iliyotamba sana miaka ya mwanzo ya 90 jijini Dar es salaam, ikifahamika kwa jina la kwaya mtakatifu Maurus kanisa Katoliki Kurasini. Kutoka kwao tumekuchagulia wimbo Yesu Akalia.
Mitaa ya Kinondoni, jijini Dar es salaam, tunakutana na kwaya ya Kinondoni kanisa la Kisabato, kwaya ambayo ilivuma sana enzi zake chini ya mwalimu wao Gideon Kasozi, kutoka kwaya hii tumekuchagulia wimbo 'Yesu Alisononeka'.
Malizia na wana Kinondoni Revival kutoka Assemblies of God, kwaya ambayo imeendelea kusimama katika utumishi kwa miaka kadhaa na kuendelea kubariki wengi. Kupitia album yao ya Mtu wa nne ambayo bado haijapata mrithi wake, tumekuchagulia wimbo uitwao 'Imekwisha'. Tunakutakia Ijumaa Kuu yenye tafakari kuu juu ya maisha yako na yangu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni