Kwa watu wa Mungu!
Watu wa Mungu, ashukuriwe Mungu atupaye uzima na ya kwamba tu hai tena kwa neema yake.
Tunalo la kujivunia lakini si katika miili hii tuliyo nayo bali kwa kuwa tumeipata neema ya Jehova.
Ndugu wapendwa imetupasa kuwa na juhudi
sana kuzidi sana katika kulijua Neno la Mungu ili tuwe na hakika na
ushindi katika hatari nyingi za dunia.
Maana ”dunia” inasema inayo mazuri,
lakini si mbele za Mungu, maana ifahamike hivi; yaliyo yote mazuri
duniani ni yaliyo mabaya mbele za Mungu na yaliyo mabaya mbele za Mungu
ni yaliyo mazuri kwa duniani, basi kila mtu na asema na akili yake
mwenyewe.
Kwa hali hiyo basi; sisi tulio kwa Mungu
sawa sawa twajua hivi, kheri uongo wa Mungu kuliko ukweli wa dunia,
maana ikiwa kwa uongo huo wa Mungu sisi tu hai rohoni tukiiponya miili
hii, basi una faida gani ukweli wa dunia ambao kwa huo tumehitirafiana
sisi kwa sisi?
Nasema tena ikiwa kwa uongo huo wa Mungu
hatukuwa wazinifu, naam hatujawa walawiti, hatujawa waasherati,
hatujawa wafiraji, je si zaidi basi ya huo ukweli wa dunia ambao katika
huo tu wanafiki?
Mwaonaje ninyi,
Maana si kwamba hatuoni ama hatusomi alama za kuenenda kwetu na kuishi
kwetu maana kila mmoja wetu yu barozi na shahidi wa nyendo zake
mwenyewe, jifunzeni katika hili.
Sikia yupo mmoja aweza sema amemaliza
kwa sababu ya huu tuuitao wokovu lakini asijue ya kwamba yu apaswa
kutambua wokovu ni mbegu iishiyo katika tunda bovu ambalo ni mwili wake
mwenyewe.
Maana miili ni kikwazo sana katika maisha ya kuuishia haki, maana tumeokoka ndiyo lakini hatujaihama miili hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni