Kiwango cha Mungu – Double Agent
UTANGULIZI.
Pamoja na mabadiliko makubwa ya nyakati
zetu katika siasa, uchumi utamaduni (maadili) na kidini. Mungu anacho
kiwango chake ambacho ndicho anakubaliana nacho katika maisha yetu. Ili
tuweze kuishi na kufiti katika mipango na makusudi yake ni lazima
tuangalie kukitunza kiwango cha Mungu katika maisha yetu.
“Kwa kuwa mimi Bwana si kigeugeu
(sibadiliki)” Malaki 3:6 Biblia inaonyesha kuwa tumeitwa na tumfananie
Mungu na kamwe si Mungu atufananie sisi. Kwa hali hiyo kama hali yetu
haifanani na Mungu wito ni sisi kubadilika na wala si Mungu abadilike
awe kama tunavyotaka sisi au rafiki zetu, mazingira yetu au jamii.
Biblia huonyesha kuwa sisi tunabadilishwa toka UTUKUFU hadi UTUKUFU.
Mungu anatunza kiwango chake na kiwango cha Mungu kinakwenda sawa sawa
na Neno lake.
Biblia huonyesha mtu hufanana na mawazo
yake. “Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo…”.Mithali
23:7 (Tafsiri ya King James hutumia kufikiri badala ya kuona katika
nafsi.) Neno la Mungu ni mawazo ya Mungu; kwa hiyo linamfunua Mungu vile
alivyo. Ili tumfananie Mungu inabidi tulitafakari Neno lake. Ndipo
litaumba picha ya ki-Mungu katika mawazo yetu. Wala tusifanye
kuifuatisha dunia na kuwaza ya dunia tu.“Wakuu wa Yuda ni kama watu
waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji” Hosea
5:10
Wito wetu ni kutunza kiwango cha Mungu.
Sisi ni vielelezo. Kiwango cha Mungu kinamtambulisha Mungu wetu katika
jamii kama Jehova Nissi. Yaani yeye ni bendera yetu. Mfano mzuri ni
jinsi Musa katika vita dhidi ya Amaleki alivyonyanyua kiwango cha Mungu
(fimbo iliyowakilisha mamlaka ya Mungu) na hapo Joshua alishinda vita.
Watumishi na viongozi wa kiroho wakinyanyua kiwango hiki ambacho ni neno
la Mungu kina Joshua (kanisa) wanashinda vita. Kiwango kikiondolewa
kanisa na taifa hupoteza mwelekeo. Kutoka 17: 11-15
DOUBLE AGENT
Kuna watu ambao katika ujasusi(
upelelezi) hufanya kazi pande zote mbili huku kila upande ukiamini
unafanyiwa kazi wenyewe. Double agent anakubalika pande zote na hulipwa
mshahara na pande zote. Na katika ujasusi huyu ndiye mtu wa hatari
ambaye akipatikana hawezi kusamehewa. Ndani ya kanisa pia wamo double
agents. Kanisa la Laodikia walionywa kuacha tabia hii mbaya.
“Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi
wala moto (wewe ni double agent);” Ufunuo 3:15 Haiwezekani kutunza
kiwango cha Mungu kisha ukaonekana kote kote. Lazima uweke msimamo na
dira itakayotambulisha matakwa na kiwango cha Mungu.
Ni lazima tufike mahali tunamtambulisha Mungu katika kila hatua ya maisha yetu kwa viwango vyaUPENDOwetu,UAMINIFU, USAFI, UVUMILIVU, UKARIMU, HURUMA, UNYENYEKEVU NA UTII.Sharti
ifikie hatua maisha yetu yanaakisi hali ya Mungu wetu. Hapo tunaweza
kuwa manabii( wasemaji wa Mungu) kwa kizazi chetu. Watu wanaotuona
wapate ujumbe wa jinsi Mungu alivyo na anavyotaka katika maisha yao.
Hatuwezi kuridhia maovu na kuchukuliana na udhaifu wa dunia hii na bado
tutegemee kuwa nuru. Mungu atusaidie kuwa watu wanaosimamia kiwango cha
Mungu katika siku zetu na hapo maisha yetu yatakuwa na faida katika
ufalme wa Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni