HEZRON MARWA MWANAFUNZI WA YESU
Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...
Siku ya leo,Bwana Mungu akuhudumie kwa namna ya tofauti tunapomalizia hii tafakari.
Kumbuka, tulikuwa tumekwamia kuchimba kiundani katika tafakari,
Tukijifunza juu ya njia moja ya kwanza ya kupokea muujiza/jibu lako kutoka kwa mwenye majibu ambaye ndie wa milele,
Ni Bwana wa mabwana,
Mfalme wa wafalme,
Mungu mwenyezi,
JEHOVA aliyekuwepo,aliyepo na atakayekuwapo milele na milele.
Tulijifunza njia moja ya kupokea jibu lako nayo hiyo njia nilikuamba ni kujisalimisha kwake BWANA.
Leo tunajifunza njia nyingine ya kupokea jibu lako.
Kumbuka kwamba,
Kila jibu juu ya swali ulilonalo lipo kwa BWANA.
Labda kabla hatujaangalia njia nyingine itupasayo kupokea majibu kutoka kwa Bwana,
Niseme hivi;
Katika njia hiyo ya kujisalimisha kwa Bwana,ipo gharama ikupasayo kuilipa.
Gharama yenyewe ni ya kuidharau aibu.
Aibu ni gharama,
Aibu hutesa maisha yetu,
Wengi,hatupokei kwa sababu ya kuwa na AIBU.
Mungu leo atusaidie sana tuweze kuidharau aibu.
Ili ujifichue na umfuate Bwana Yesu,lazima ukubali kuacha yote.
Tazama sasa;
jamii inayokuzunguka itakusema vibaya,kwa sababu ya kumfuata Bwana Yesu.
Kujisalimisha kwa Bwana Yesu ni kuokoka.
*kuokoka ni kukutana na Yesu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni