Powered By Blogger

Jumanne, 6 Mei 2014

WAIONAYO NJIA YA UZIMA NI WACHACHE SANA.



Njia iendayo katika mateso ya moto ni pana sana na waingiao ni wengi sana.Si wote waimbao kwaya,kushika biblia n.k waendao mbinguni.Mathayo 7:21 

wengi wenye majina makubwa makubwa hata wengine ni wachungaji,mapadre mashehe, maraisi, mawaziri n.k watakwenda njia ile pana.

Ni wachache sana waendao mbinguni.Hatupaswi kuridhika tu kuhudhuria ibada kama hii kwani hata shetani anaingia kwenye nyumba za ibada Ayubu 1:6 .

Si swala la kumwabudu MUNGU mmoja kwani pia mashetani hufanya hayohayo tena kwa kutetemeka.Yakobo 2:19.

Moto wa milele uliubwa kwa ajili ya shetani na malaika zake na MUNGU hakukusudia kabisa kumwachilia mwanadamu aende huko.Lakini wengi wanakwenda huko kwa kukosa maarifa ama kufuata tu mkumbo.Mtu anakuja kanisani kwa lengo tu Fulani mfano kuwafuata wazazi kutafuta misaada ama fedha,wachumba ,kazi ,chakula n.k na ukimpima katika mizani ya utakatifu utakuta hayupo yupo duniani kabisa.

Lazima tufahamu kuwa kuna maisha baada ya hapa duniani na hatutaishi hapa duniani milele na milele.Hapa sisi wote ni wasafiri na wapitaji.Mathayo 25:41.Tuwe macho tusije tukaaibika kama wale wasio na matumaini.Tusifuate tu mkumbo jiulize endapo kweli umeokoka.

BWANA YESU pekee ndiye anayeokoa(Yohana 14:6)

Soma kwa makini kisha ''Share'' kwa marafiki zako kwani utawaponya wengi ili wampe YESU maisha yao na kuokolewa.

MUNGU akubariki sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni