Jumanne, 3 Desemba 2013
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZA MWILI WA MAREHEMU PAUL WALKER WA FAST AND FURIOUS ULIVYOONYESHWA
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
HII NDIO INTERVIEW YA YULE SHUJAA WA WESTGATE AMBAYE NI KIVUTIO CHA WATU WENGI HIVI SASA
Ukiachana na ushujaa wake wa kujitoa kuwasaidia watu walikuwa ndani ya lile jengo, kitu cha kwanza kilichomvuta kwenda mle ndani ni ndugu yake wa pekee wa kiume alikuwa ndani humo. Lakini alivyofika ndani na ndugu yake kufanikiwa kutoka alipatwa na hasira za kuendelea kuwasaidia wengine.Angalia interview hii na ambayo anasimulia kila kitu
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
HEZZO Radio Tanzania
- Your Official Sheng Station, Streaming Live 24/7 From Nairobi, Kenya. Follow us on Facebook and Google+! Twitter @Ghettoradio895
Rate this track
votes
- African Hit Radio 24/7 Os babo's - Dia Mapuca (Afro)
- Ghetto Radio Nairobi null - null
- African Classics Radio Tabu Ley Rochereau - Mireille Mwana
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Jumatatu, 2 Desemba 2013
TAZAMA TWEET YA TYRESE,VIN DIESEL NA LUDACRIS MARA BAADA YA KIFO CHA PAUL WALKER WA FAST AND FURIOUS..!!
Katika hali ya simanzi na maumivu makubwa, hii ndiyo tweet aliyoandika
Vin Diesel mara baada ya mshikaji wake na swahiba wake mkubwa Paul
Walker kufariki kwa ajali ya Gari iliyotokea jumamosi mchana
Dwayne Johnson, "who starred in Fast 5 and Fast & Furious 6 , and was filming the seventh film with Paul, took to Twitter sharing his heartbroken reaction":
Ludacris, "who has starred in two Fast & Furious films
(plus the one they were filming) with Paul posted a sweet photo of the
cast holding hands around a dinner table, with “Thankful for the family”
written on the picture:
hizi ni post za tyrese gibson kwenye page yake ya facebook
tyrese akiwa na Paul Walker
hizi ni post za tyrese gibson kwenye page yake ya facebook
I will keep your energy with me forever #AshesOfAnAngel
fast family around the world we love you and we love you Paul is the
heartbeat of this franchise and were gonna see to it that his energy and
presence lives on forever #myhearthurtssobad
My heart is hurting so bad
no one can make me believe this is real
Father God I pray that you send clarity over this cause I just don't understand
My heart hurts it's broken no one can convince me that this is real.... Prayer warriors please pray real hard for his only child, his daughter and family... #HeartOfAnAngel13YrsFamilyForever WeJustCelebreatedYour40thBirthday..... My God... My God... I can't believe I'm writing this
no one can make me believe this is real
Father God I pray that you send clarity over this cause I just don't understand
My heart hurts it's broken no one can convince me that this is real.... Prayer warriors please pray real hard for his only child, his daughter and family... #HeartOfAnAngel13YrsFamilyForever WeJustCelebreatedYour40thBirthday..... My God... My God... I can't believe I'm writing this
tyrese akiwa na Paul Walker
Tulikupenda ila mungu kakupenda zaidi.. R.I.P Paul
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Jumatano, 27 Novemba 2013
KWA TAARIFA YAKO : JE UNAJUA WAIGIZAJI NYOTA FILAMU YA SAMSON NA DELILAH NI MAREHEMU?
Victor John Mature a.k.a Samson.©Wikipedia |
KWA TAARIFA YAKO hii leo tunakujuza kwenye mambo ya uigzaji kama tulivyokujuza kuhusu mwigizaji wa filamu ya Yesu, na watu kuanza kuuliza kama mwigizaji huyo bado yupo jibu ni ndiyo mwigizaji huyo bado yupo hai kwakuwa Tarifa za wakristo haijawahi kusikia kifo chake ikiwa pamoja na mtandaoni hakuna taarifa zilizoandikwa juu ya kifo chake. Sasa hii leo KWA TAARIFA YAKO je unajua waigizaji wakuu wawili wa filamu ya Samson na Delilah iliyoigizwa mwaka 1949 wote wawili kwasasa ni marehemu?
KWA TAARIFA YAKO aliyeigiza kama Samson jina lake kamili ni Victor John Mature mzaliwa wa mji wa Louisville, Kentucky nchini Marekani alifariki mwezi August,1999 kwa ugonjwa wa kansa ya damu (Leukemia) akiwa na miaka 86 mwigizaji huyu mwenye asili ya Uitaliano ambako ndiko baba yake mzazi alitokea mama yake akiwa mzaliwa wa Marekani mwenye asili ya Uswisi. KWA TAARIFA YAKO kazi ya uigizaji aliianza mwaka 1939 na kustaafu mwaka 1984. Mwigizaji huyu ambaye ana historia ya kipekee kwakushiriki vita kuu ya pili ya dunia kabla ya kustaafishwa inaelezwa licha ya kushiriki katika filamu tofauti alipata mafanikio zaidi katika kuigiza habari za Biblia hususani filamu ya Samson na Delilah.
Hedy Lamarr a.k.a Delilah©Wikipedia. |
Alipata uraia wa Marekani mwaka 1953 akiwa na miaka 38. KWA TAARIFA YAKO mwigizaji huyu pia anarekodi nyingi katika safari yake ya uigizaji lakini wako sambamba na mwigizaji mwenzake marehemu Victor ama Samson katika suala la mahusiano maana yeye kaachika mara sita na katika mbili ya ndoa hizo alibahatika kupata watoto watatu mmoja kati yao alimuasili.
JIKUMBUSHE UONE JINSI WALIVYOKUWA MARIDADI KATIKA UIGIZAJI
KWA TAARIFA YAKO Hedy ama Delilah kama alivyoigiza alianza rasmi kazi ya uigizaji mwaka 1930 na kustaafu mwaka 1958. Kifo cha mwigizaji huyo kilitokana na matatizo ya moyo ambapo alifia nyumbani kwake huko Casselberry Florida ambapo mtoto wake Anthony Lodar alichukua majivu ya mama yake na kwenda kuyapeperusha kwenye msitu wa Vienna nchini Austria kama mama yake alivyotaka iwe endapo akifariki.
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO vinginevyo tukutane wiki ijayoooo….. uchambuzi huu pamoja na picha ni kwahisani ya mtandao wa Wikipedia.
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
shalom ndugu wapendwa...jina la Bwana wetu Yesu Kristo lipewe sifa...
jamani ndugu zangu nimeona ni vyema tukashare yale ambayo jana katika ibada niliweza kuyapata.
alihubiri askofu Mwaipopo,na ilikiwa ni muendelezo wa masomo ya kitabu
cha Marko.jana ilikuwa Marko 8: 22-38. (pia tulisoma na Luka 9: 23 - 27)...
hapo nilipata mambo mawili ya muhimu:
1:- Unapokuwa katika jambo lolote,hakikisha unakuwa wa rohoni na
mwilini pia...hii itakuwezesha kutambua yaayoendelea.mf,unakutana na
mtu unamsalimia kwa kumpa heshima yake,yeye anakujibu kuwa wewe ni mtu
mkubwa sana na hustahili kumuamkia...hapo katika roho utatambua kuwa
huyo ni wa ulimwengu mwingine na kujua kuwa amegundua uliye naye ni
mkuu kuliko huyo wa ulimwengu wake(shetani).
2:- Kumbuka kujikana kwa ajili ya Mungu
-hii ni kuacha yaliyo matakwa/mapenzi yako na kutimiza au kufanya yaliyo mapenzi ya Mungu
ni hayo tu ndugu zangu,na Bwana Yesu awabariki.
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Jumapili, 24 Novemba 2013
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Jumanne, 19 Novemba 2013
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Jumatatu, 18 Novemba 2013
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Tunasoma; "Katika shida yangu nalimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi." Zab 118:5, (Andiko la kusimamia fundisho hili)
Mtunga Zaburi anajaribu kuelezea pale alipopata shida,alimuita Bwana,Bwana akamjibu.
Ikiwa Bwana alimjibu basi Yeye BWANA ndie JIBU wa tatizo lake.Sikia hapo,
alipokuwa na shida -hakuwa katika nafasi ya ki-ungu,yaani ile nafasi ambayo anastahili kuwapo,
ndio maana BWANA alipomjibu kitu cha kwanza AKAMWEKA PANAPO NAFASI.
Mtu mwenye shida hana nafasi,
ili awe na nafasi yambidi aliitie jina la BWANA ili BWANA mwenye kutoa nafasi ampatie nafasi.
Nafasi katika ulimwengu wa roho ni KIBALI.
Oooh kumbe !;
Kibali chatoka kwa BWANA,na kumbe kibali kipo tayari kwa ajili yetu, pale tutakapomuita BWANA,BWANA atatujibu na kukiachilia kibali mbele zetu.
Basi Ikiwa ndio hivyo BWANA ndie JIBU na mtatuaji wa kila aina ya shida.
Nakusalimu mpendwa,
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya…
Nasema Haleluya….
Jina la BWANA lisifiwe…
Tulikuwa tunaangalia njia ya kwanza ya kupokea majibu yako kutoka kwa Yeye Mungu mwenye majibu.
Na nilikuambia njia ya kwanza ni ;
Kujisalimisha kwa Bwana Yesu.
Na hapo tuliona watu wachache wenye akili ambao walimfichua mtu bubu mwenye pepo kwa kumpeleka kwa BWANA,
BWANA akamponya,
naye huyo bubu akanena kwa mara ya kwanza ,kisha makutano wakastaajabu.
Maana haikuwahi kuonekana katika Israeli wakati wote
(Mathayo 9 :32-33)
Kumbuka;
Yule bubu asin’geponywa kama asing’epelekwa kwa BWANA.
Watu walipoona yafaa kumpeleka,Wakampeleka mbele za Bwana,Naye akapokea uponyaji saa ile ile.
Nasi yatupasa kuwaleta wenye mapepo,magonjwa,wadhaifu,N.K
Wote hawa hawawezi kumwendea BWANA wao kama wao,muda mwingine yatupasa KUWAPELEKA ndipo waponywe.
Ili umpeleke mgonjwa kwa Bwana,Hakikisha kwanza wewe mwenyewe sio mgonjwa. Yaani uwe safi,
safi katika kila eneo,
uwe safi hata katika kinywa,
maana mgonjwa anahitaji maneno ya faraja
Kwa kumuambia mfano;
'' Utapona tu,yupo Yesu wa Nazareti asiyeshindwa na ilo tatizo lako.,…Polee mpendwa,hayo ni ya kawaida kabisa,mpe maisha BWANA Yeye atakutua mzigo wako…N.K ''
-Lakini sio uwe na maneno ya kumvunja moyo.
Haleluya…
Tuwapeleke wagonjwa kwa BWANA ambaye Yeye ni JIBU na mtatuaji wa kila aina ya shida.
Tuangalie mfano mwingine mmoja katika siku ya leo kwa habari ya KUJISALIMISHA KWA BWANA.
Nimekuambia kwamba,hiyo ndio njia ya kwanza ya kupokea uponyaji wako,
Na hapa tunasoma,
Marko 5:27-28,&34
'' aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.
34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.’’
Haleluya…
Huyu ni mwanamke aliyetokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, Alafu sio tu kutoka damu,sikia, Biblia inasema aliteswa sana kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.
*Oooh,Jesus,I’ve mercy on us…
Unajua watu wengi wakisoma maandiko kama haya yenye kuelezea shida za watu kama hizi,wanafikiri kwamba ilikuwa rahisi….
Mimi nasema hapana,
Haya mazingira tunayoyasoma katika maandiko matakatifu ni mazingira magumu sana,
Tazama habari hiyo hapo juu ya huyo mwanamke aliyetokwa na damu muda mlefu namna hiyo pasipo kupona na pia alipoteza mali zake zote,nasema alipoteza mali zake zotee,sio mali kidogo bali ni mali zake zote zilipotea,
na hata hapo bado hakukumfaa kitu.
Sasa utaona ni jinsi gani alivyokuwa akiteseka huyu mwanamke.
Lakini leo anatuambia habari njema maana haumwi tena,
Hateseki tena,
Hana msiba tena,
Maana amemwendea mmoja mwenye majibu juu ya tatizo lake la kutokwa damu.
Ni Yesu pekee ambaye ndie daktari wa kweli,
Yeye ni bingwa wa mabingwa.
Nalikuambia tunajifunza njia moja tu ya kupokea muujiza/uponyaji wako na ni
KUJISALIMISHA KWA BWANA.
Mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu muda mlefu huo,Yeye alipoijua siri hii ya uponyaji,
kwamba uponyaji halisi upo mbele za BWANA,alifunga safari na kumuendea mahali alipo BWANA.
Biblia inasema
'' aliposikia habari za Yesu,
alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;’’ Marko 5 :27
Sikia sasa,
Huyu mwanamke alikuwa ana akili nyingi sana,
Maana yeye alihitaji kwanza KUSIKIA HABARI ZA YESU.Kisha aliposikia AKACHUKUA HATUA kwa kupita kwa nyuma ya mkutano na kuligusa vazi lake.
Tazama hapo kwa makini Biblia inasema '' Aliposikia…'' IMANI ya mwanamke huyu ilianzia hapo kwa kusikia habari za Yesu Kristo.
Na mara tu baada ya kusikia AKAPIGA HATUA,
Hii ikimaanisha kwamba ALIPOKUWA NA IMANI AKAJUMLISHA NA MATENDO ya kugusa pindo la vazi la BWANA. Naye akapona na ule msiba saa ile ile.
Hizo hatua alizozichukua mwanamke huyu,ndizo hatua tutakazojifunza katika fundisho lijalo…
ITAENDELEA…
• Usikose fundisho lijalo mahali hapa,ambapo tutachimba zaidi.
Kwa maombezi;
• +255 767 674 089
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
COMPUTEC TRAINING COMPUTER WANAKULETEA COURSE ZA COMPUTER NYOTE MNAKARIBISHWA
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Mtumishi Cosmas Chidumle akihubiri
Mtumishi Cosmas Chidumle akihubiri
Kama ilivyo katika mkutano mwisho
alisimama Gwiji la Mziki(Mwana Mziki
halisi) ambae kwa sasa anamtangaza Yesu kwa Nguvu zake Mwinjilisti
Cosmas Chidumle. Aliwaambia wakazi wa Vijibweni kuwa Kama ni Uhuni yeye
alikuwa Mhuni zaidi, kama ni usharobaro basi alikuwa hivyo ila wa enzi
hizo. Pamoja na maisha ya kujulikana aliyoyaishi kipindi hicho hakuwa na
furaha kwani alikuwa amepungukiwa kitu. Yesu alipoingia katika maisha
yake maisha yake yamekuwa ya tofauti sana. Mwinjilisti huyo aliutumia
dakika kumi kuhubiri kutokana na kuchelewa kufika lakini hio ilikuwa
Ijumaa lakini Jumamos Mungu anaenda kutembea kwa njia ya ajabu ambapo
Mtumishi atasimama mapema na watu kwenda kufunguliwa.
Katika mkutano huo watu walimkubali
Bwana Yesu na kuongozwa sala ya toba.
MKUTANO HUU UNALETWA NA KANISA LA T.A.G.
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
UKRISTO/UISLAM
HEZRON MARWA MWANAFUNZI WA YESU |
UKRISTO
Wakristo tunaamini kwamba Yesu ni
mwana wa Mungu, aliteswa, alikufa na siku ya tatu alifufuka na pia
tunaamini ndiye njia ya kutufikisha mbinguni na alipopaa kwenda mbinguni
aliahidi kuleta msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu!
UISLAM
Ndugu Waislamu huamini ALLAH ndio Mungu,
Yesu sio mwana wa Mungu, alikuwa mmoja wa mitume wakubwa, alifanya
miujiza lakini hakufa msalabani ni““Hawakumuua wala hawakumsulubisha lakini
walidhani wamefanya hivyo (Quran 4:156) “Mungu alimuinua …….(Quran
4:157).
—–KWA WALE WANAOTAKA KUJUA UKWELI
KARIBUNI— MAWASILIANO +255 767 674 089
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
MAOMBEZI KWA JINA LA YESU YAKIFANYIKA NA WATU KUFUNGULIWA KUTOKA NGUVU ZOTE ZA GIZA ZILIZOKUWA ZIMEWAFUNGA
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Kwanini nguvu za kanisa la kwanza hazionekani katika kanisa la leo?
Kwanini nguvu za kanisa la kwanza
hazionekani katika kanisa la leo?
Naianza
mada mpya kwa swali gumu na linaloweza kuibua mijadala mingi huko
tuendako;
lakini ambayo itakuwa ni changamoto historia ya kanisa sanjari na
madhehebu ya
Kikristo yaliyopo ulimwenguni kwa sasa. Kwa wasomaji wangu wa miaka
mingi,
mtakumbuka huko nyuma, niliwahi kuandika makala yenye kuchambua tofauti
zilizopo kati ya “madhehebu ya Kikristo” na “Ukristo halisi”.
Ninalazimika
kurudi katika uchambuzi wenye mwelekeo huo; lakini lengo kamili likiwa
ni
kudhihirisha kimaandiko na kihistoria kuhusu kitendawili cha miaka mingi
kuhusu
tofauti kubwa iliyopo kati ya nguvu za kanisa la kwanza na udhaifu wa
kanisa la
leo. Najua kuna utetezi ambao umekuwa ukitolewa na kurasimishwa kama ndio sababu kamili. Lakini matukio ambayo
yamejitokeza katika karne za hivi karibuni yanaufanya utetezi uliokuwepo
kupoteza ushawishi; na hivyo kutoa mwanya wa kufanya upya utafiti wa
kimaandiko
na kihistoria; ili kupata majibu sahihi ambayo hayatapingika hata kama yasiyopokubaliwa kwa haraka. Katika kujenga
msingi
thabiti wa mada hii, nitaanza kwa muhtasari kuchambua kwanza tofauti
kati ya
“Ukristo” na “Madhehebu ya Kikristo”:
Tafsiri ya misamiati ya “Ukristo”
na “Madhehebu ya Kikristo”
Kwa msomaji mpya unaweza kudhani
ninataka kukuchanganya kwa kusema kuna tofauti ya Ukristo halisi na
Madhehebu
ya Kikristo. Pengine wewe unafikiri vyote ni kitu kile kile, chenye
maana moja,
ila majina tu ndiyo yanatofautiana. Tusisahu pia kwamba tofauti za
maneno
zinatosha kuleta maana tofauti ya maneno husika. Nivumilie tu nijieleze
ili
unielewe na kujua kule ninakoelekea.
Tafsiri ya awali nainukuu katika Kamusi
ya Kiswahili Sanifu, ili kupata maana ya maneno mawili ambayo, ni
“Ukristo” na
la pili “Madhehebu”. Maana za maneno haya zitatupa picha ya tofauti
zilizopo
kisha tunaendelea na uchambuzi kutoka vyanzo vingine vya lugha.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu imelitafsiri
neno “Ukristo” kuwa ni: “Dini inayoamini
kuwa Mungu ni mmoja, inayofuata mafundisho ya Yesu Kristo.”
Hapa neno Ukristo limetafrisiwa
kuwa ni dini.
Hapa inaonesha kwamba Ukristo umejumuishwa na dini nyingine kama vile Uislamu na Ubudha.
Tunapokuja kwenye msamiati wa neno
“Madhehebu” tunakuta Kamusi ya Kiswahili Sanifu imelitafsiri katika
maana tatu
zifuatazo: 1. Fikira na mwongozo wa
kidini unaotokana na uelewaji wake wa misingi ya dini hiyo na unaoleta
tofauti
ndogondogo za mawazo lakini zisizovunja misingi ya dini hiyo. 2. Wafuasi
wa
mawazo ya kiongozi wa dini. 3. Mwenendo fulani wa kufanya au kuendesha
mambo.
Tukichukua tafsiri ya kwanza na
kuihusisha na msamiati wa madhehebu ya Kikristo inaweza kusomeka kama ifuatavyo: “Madhehebu
ya Kikristo ni fikira au miongozo ya kidini inayotokana na uelewaji wake
wa
misingi ya dini ya Kikristo na inayoleta tofauti ndogondogo za mawazo
lakini
sizizovunja misingi ya dini hiyo ya Kikristo.”
Tukichukua tafsiri ya pili na
kuihusisha na msamiati wa madhehebu ya
Kikristo inaweza kusomeka kama
ifuatavyo:
“Wafuasi wa mawazo ya viongozi waasisi wa
madhehebu katika dini ya Kikristo.”
Mpaka hapo, tukizichukua maana za
maneno yaliyotajwa ya, “fikira”, “Mawazo” “Miongozo inayoleta tofauti
ndogondogo za mawazo” tunaweza kufikia muafaka kwamba maana ya jumla ya
Kiswahili kuhusu madhehebu ya Kikristo inaweza kusomeka kama
ifuatavyo: “Itikadi za kimakundi
zilizoasisiwa na viongozi mbali mbali wa madhehebu ya Kikristo
yanayotumia
mwavuli wa dini ya Kikristo”
Tukiishia katika maana iliyotokana na
Kamusi ya Kiswahili Sanifu, tutakomea katika uelewa kwamba, madhehebu ya
Kikristo na Ukristo ni kitu kimoja lakini chenye tofauti ndogondogo
zinazotokana na mawazo ya viongozi wa makundi husika.
Je! Hii ndio maana yake halisi? Je!
Tafsiri ya Kiswahili iliyopo imechukua maana sahihi ya maneno husika
kutoka
kwenye vyanzo sahihi vya lugha nyingine zilizotangulia kutumia maneno
haya?
Kimsingi, tukitaka kujua maana sahihi
ya neno, hususani lile lililoazimwa kutoka katika lugha nyingine, ni
muhimu
kurejea kwenye lugha asilia na kujifunza matumizi asilia ya neno hilo kabla
halijahamishiwa katika lugha nyingine. Na hii ndiyo kazi nataka tuifanye
hivi
sasa katika uchambuzi wa maneno ya “Ukristo” na “Madhehebu ya Kikristo”
jinsi
yalivyotangulia kutumika kwenye lugha asilia kabla hayajahamishiwa
katika
Kiswahili chetu.
Chimbuko la msamiati ya “Ukristo”
Katika maandiko matakatifu ya Agano
Jipya hakuna msamiati wa neno “Ukristo”. Kuna maneno mawili yafuatayo:
1.
Kristo, na 2. Mkristo. Maana ya neno la kwanza la Kristo ni “Christos”
likimaanisha “mpakwa mafuta”. Neno la pili la
“Mkristo” kwa lugha asilia ni: “Christianos”
likimaanisha “mfuasi wa Kristo”. Neno
hili lilitajwa kwa mara ya kwanza mnamo karne ya pili ambapo watu wa
mataifa
waliamua kuwaita wenye kumwabudu Yesu kuwa ni “Wakristo”
“hata alipokwisha kumwona akamleta
Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa
na
kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo
Antiokia.”
(Mdo.11:26)
Mara ya pili tunakutana na msamiati wa
neno “Mkristo” wakati Paulo alipokuwa
akijitetea mbele ya kiongozi katika dola ya kirumi jina lake Agripa .
Huyu alisikiliza utetezi wa kiimani wa Paulo akajikuta anashawishiwa
kufanyika
mfuasi wa Kristo mpaka akamwonya Paulo kwa maneno yafuatayo:
“Agripa akamwambia Paulo, kwa maneno
machache wadhani kunifanya Mkristo.” (Mdo.26:28)
Mara ya tatu tunakutana na msamiati wa
neno “Mkristo” wakati Petro alipokuwa
akiwausia na kuwatia moyo wafuasi wa Kristo ili kila Mkristo atetee
imani yake
hata kama yu katika mateso isivyo
halali:
“Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo
asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo .” (1 Pet.4:16)
Kufuatia nukuu za maandiko kuhusu
msamiati wa neno “Ukristo” tumebaini
neno hili halijaandikwa kwenye nyaraka za Agano Jipya. Badala yake
tumekutana
na maneno ambayo yanafanana na huenda ndiyo yaliyosababisha kuzaliwa kwa
msamiati wa neno “Ukristo”.
Hapa tunajifunza kwamba, msingi na
chimbuko la “Wakristo” na “Mkristo” ni Yule mwenye jina hilo tangu mwanzo
ambaye
ni Yesu Kristo. Huko Antiokia, wanafunzi wa Yesu, badala ya kuendelea
kuitwa
kwa jina refu la wanafunzi wa Yesu Kristo” wakapewa jina fupi la ”Wakristo”
lenye kuonesha moja kwa moja
mahusiano yaliyopo ya kiimani kati yao
na Kristo mwenyewe. Huko Baadaye neno “Mkristo”
lilitumika kumtambulisha mwamini mmoja mmoja.
Katika historia ya mwanzo wa matumizi
ya maneno haya “Wakristo” na “Mkristo” hatusomi habari za “mawazo” au
“itikadi
za kimakundi” katika imani ya Kikristo. Waliotajwa kutumia maneno haya
hatusomi
kwamba yalikuwa ni majina ya kimakundi au kiitikati zenye “tofauti
ndogondogo”
za mawazo ya waasisi wa kiimani. Ni maneno yaliyobadilika kuwa majina ya
kundi
lile lile moja, lenye imani moja, ubatizo mmoja, Bwana mmoja, ambalo
lilikuwa
likiongezeka idadi na kuenea katika miji na nchi mbali mbali za
ulimwengu wa
karne ya kwanza.
Kwa bahati mbaya, katika nyaraka za
asili za Agano Jipya, hatuna msamiati wa neno, “madhehebu ya Kikristo”
kwa
maana ya tafsiri ile tuliyoipata kwenye Kiswahili chetu isemayo: “Itikadi
za kimakundi zilizoasisiwa na
viongozi mbali mbali wa madhehebu ya Kikristo yanayotumia mwavuli wa
dini ya
Kikristo”
Kwa mantiki hii, kinachoweza kutusaidia
kujua chimbuko la msamiati wa madhehebu ya Kikristo kwa maana ya
“itikadi za
kimakundi” katika imani ya Kikristo, si kingine bali ni historia ya
kanisa,
ambayo tunaendea kuipitia kwa ufupi kama
ifuatavyo:
Chimbuko la “Madhehebu ya Kikristo”
Katika karne za kwanza za historia ya
Ukristo, hakukuweko kabisa “madhehebu ya Kikristo” kama
tuliyo nayo hivi leo. Japokuwa zilijitokeza changamoto za kuibuka kwa
vijikundi
vilivyokuwa vikijimega, vingi vilikuwa vidogo na wafuasi wake waliitwa
“Wazushi” wala hawakuhesabiwa kuwa ni sehemu ya Ukristo. Tangu kipindi
cha
mwanzo wa Ukristo kulikuwepo kanisa moja
tu la “Katoliki” kwa maana ya “kanisa la ulimwengu mzima”. Kimsingi,
mwamini
yeyote ambaye hakuwa mshirika katika kanisa hilo hakutambuliwa kuwa ni Mkristo.
Historia ya “Madhehebu ya Kikristo”
inaanza na kitu kinachoitwa “Mgawanyiko wa kanisa”. Mngawanyiko wa
kwanza
mkubwa ulijitokeza kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1054 uliotokana na “Great
Schism” kati ya Kanisa la
Mashariki na Kanisa la Magharibi. Kuanzia hapo kukawepo makundi makubwa
mawili
ya kikristo ambayo baadaye yalikuja kujulikana kama
Kanisa Katoliki la Magharibi na kanisa la Mashariki la Orthodox
Mgawanyiko mkubwa wa pili wa kanisa
ulitokea
katika karne ya 16 wakati wa Matengenezo
Kiprotestanti ambayo mwasisi wake alikuwa Martin Luther. Katika
kuonesha
kutokuridhishwa kwake na mwenendo wa imani ya Kanisa mnamo mwaka 1517
alichapisha na kubandika mambo 95 (Thesis)
ambayo hatimaye mnamo mwaka 1529 yalianzisha rasmi vuguvugu la
Uprotestanti.
Hoja ya msingi iliyoleta mgawanyiko ni
madai ya uhuru wa kuyatafsiri mambo ya imani na wokovu wa Mungu kama jambo linalomhusu mtu binafsi na Mungu,
pasipo
kupitia kwa mtu au taratibu za kitaasisi zenye kusimamiwa na binadamu.
Katika kuweka mkazo wa jinsi hii, wa
uhuru wa kila mtu kujitafsiria maandiko na kusimama mbele za Mungu kwa
imani
yake, kukaligawa kanisa na kuwa na makundi mawili ambayo ni
“Uporotestanti” na
“Ukatoliki”. Kundi la Ukatoliki likaendelea na msimamo wake kwamba wa
tafsiri
ya maandiko na mafundisho kuwa chini ya udhibiti wa utawala wa kanisa
ili
kuepusha kuwachanganya wafuasi kwa sababu ya kila mtu kujitafsiria mambo
yake
binafsi.
Kundi lililomeguka kutoka kwenye
“Ukatoliki” lenyewe likaendeleza vuguvugu lake jipya
la kupinga kwamba utaratibu wa kudhibiti tafsiri ya maandiko tayari
kulikwisha
kusababisha uharibifu wa imani ya kweli ya Ukristo. Likaendelea
kusisitiza
kwamba waamini wapewe uhuru wa kujisomea maandiko wenyewe na
kuyatekeleza kwa jinsi
wanavyoongozwa na dhamiri zao wenyewe.
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Kwanini nguvu za kanisa la kwanza hazionekani katika kanisa la leo?
KUELIMISHA JAMII, KUELEWA JUU YA TECHNOLOGIA YETU KWA SASA.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)