Powered By Blogger

Jumatano, 27 Novemba 2013

KWA TAARIFA YAKO : JE UNAJUA WAIGIZAJI NYOTA FILAMU YA SAMSON NA DELILAH NI MAREHEMU?


Haya msomaji wetu wa Hezron Mwanafunzi wa Yesu  karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya Tarifa za wakristo kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini Tarifa za wakristo ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


Victor John Mature a.k.a Samson.©Wikipedia

KWA TAARIFA YAKO hii leo tunakujuza kwenye mambo ya uigzaji kama tulivyokujuza kuhusu mwigizaji wa filamu ya Yesu, na watu kuanza kuuliza kama mwigizaji huyo bado yupo jibu ni ndiyo mwigizaji huyo bado yupo hai kwakuwa Tarifa za wakristo haijawahi kusikia kifo chake ikiwa pamoja na mtandaoni hakuna taarifa zilizoandikwa juu ya kifo chake. Sasa hii leo KWA TAARIFA YAKO je unajua waigizaji wakuu wawili wa filamu ya Samson na Delilah iliyoigizwa mwaka 1949 wote wawili kwasasa ni marehemu?

KWA TAARIFA YAKO aliyeigiza kama Samson jina lake kamili ni Victor John Mature mzaliwa wa mji wa Louisville, Kentucky nchini Marekani alifariki mwezi August,1999 kwa ugonjwa wa kansa ya damu (Leukemia) akiwa na miaka 86 mwigizaji huyu mwenye asili ya Uitaliano ambako ndiko baba yake mzazi alitokea mama yake akiwa mzaliwa wa Marekani mwenye asili ya Uswisi. KWA TAARIFA YAKO kazi ya uigizaji aliianza mwaka 1939 na kustaafu mwaka 1984. Mwigizaji huyu ambaye ana historia ya kipekee kwakushiriki vita kuu ya pili ya dunia kabla ya kustaafishwa inaelezwa licha ya kushiriki katika filamu tofauti alipata mafanikio zaidi katika kuigiza habari za Biblia hususani filamu ya Samson na Delilah.
Hedy Lamarr a.k.a Delilah©Wikipedia.
KWA TAARIFA YAKO kitu kingine kilichomfanya apate mafanikio katika uigizaji manabii inaelezwa kwamba muonekano wake ulichangia sana akidaiwa kuwa alikuwa na muonekano wa kitakatifu. Kitu kimojawapo cha mwigizaji huyu katika maisha yake aliwahi kuoa na kutoa talaka mara tano mwe!. Kwa upande wa mwigizaji mwenza mwanamama mrembo Hedwig Eva Maria Kiesler Lamar mzaliwa wa Vienna Austria na Hungary  wazazi wake wakiwa ni wayahudi alifariki dunia mwezi Januari mwaka 2000 akiwa na miaka 85.

Alipata uraia wa Marekani mwaka 1953 akiwa na miaka 38. KWA TAARIFA YAKO mwigizaji huyu pia anarekodi nyingi katika safari yake ya uigizaji lakini wako sambamba na mwigizaji mwenzake marehemu Victor ama Samson katika suala la mahusiano maana yeye kaachika mara sita na katika mbili ya ndoa hizo alibahatika kupata watoto watatu mmoja kati yao alimuasili.

       JIKUMBUSHE  UONE JINSI WALIVYOKUWA MARIDADI KATIKA UIGIZAJI




KWA TAARIFA YAKO Hedy ama Delilah kama alivyoigiza alianza rasmi kazi ya uigizaji mwaka 1930 na kustaafu mwaka 1958. Kifo cha mwigizaji huyo kilitokana na matatizo ya moyo ambapo alifia nyumbani kwake huko Casselberry Florida ambapo mtoto wake Anthony Lodar alichukua majivu ya mama yake na kwenda kuyapeperusha kwenye msitu wa Vienna nchini Austria kama mama yake alivyotaka iwe endapo akifariki.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO vinginevyo tukutane wiki ijayoooo….. uchambuzi huu pamoja na picha ni kwahisani ya mtandao wa Wikipedia.

shalom ndugu wapendwa...jina la Bwana wetu Yesu Kristo lipewe sifa...


jamani ndugu zangu nimeona ni vyema tukashare yale ambayo jana katika ibada niliweza kuyapata.

alihubiri askofu Mwaipopo,na ilikiwa ni muendelezo wa masomo ya kitabu cha Marko.jana ilikuwa Marko 8: 22-38. (pia tulisoma na Luka 9: 23 - 27)...

hapo nilipata mambo mawili ya muhimu:
1:- Unapokuwa katika jambo lolote,hakikisha unakuwa wa rohoni na mwilini pia...hii itakuwezesha kutambua yaayoendelea.mf,unakutana na mtu unamsalimia kwa kumpa heshima yake,yeye anakujibu kuwa wewe ni mtu mkubwa sana na hustahili kumuamkia...hapo katika roho utatambua kuwa huyo ni wa ulimwengu mwingine na kujua kuwa amegundua uliye naye ni mkuu kuliko huyo wa ulimwengu wake(shetani).

2:- Kumbuka kujikana kwa ajili ya Mungu
-hii ni kuacha yaliyo matakwa/mapenzi yako na kutimiza au kufanya yaliyo mapenzi ya Mungu

ni hayo tu ndugu zangu,na Bwana Yesu awabariki.
 

Jumatatu, 18 Novemba 2013


Tunasoma; "Katika shida yangu nalimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi." Zab 118:5, (Andiko la kusimamia fundisho hili)


Mtunga Zaburi anajaribu kuelezea pale alipopata shida,alimuita Bwana,Bwana akamjibu.
Ikiwa Bwana alimjibu basi Yeye BWANA ndie JIBU wa tatizo lake.Sikia hapo,
alipokuwa na shida -hakuwa katika nafasi ya ki-ungu,yaani ile nafasi ambayo anastahili kuwapo,
ndio maana BWANA alipomjibu kitu cha kwanza AKAMWEKA PANAPO NAFASI.

Mtu mwenye shida hana nafasi,
ili awe na nafasi yambidi aliitie jina la BWANA ili BWANA mwenye kutoa nafasi ampatie nafasi.
Nafasi katika ulimwengu wa roho ni KIBALI.

Oooh kumbe !;
Kibali chatoka kwa BWANA,na kumbe kibali kipo tayari kwa ajili yetu, pale tutakapomuita BWANA,BWANA atatujibu na kukiachilia kibali mbele zetu.
Basi Ikiwa ndio hivyo BWANA ndie JIBU na mtatuaji wa kila aina ya shida.

Nakusalimu mpendwa,
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya…

Nasema Haleluya….
Jina la BWANA lisifiwe…

Tulikuwa tunaangalia njia ya kwanza ya kupokea majibu yako kutoka kwa Yeye Mungu mwenye majibu.
Na nilikuambia njia ya kwanza ni ;
Kujisalimisha kwa Bwana Yesu.

Na hapo tuliona watu wachache wenye akili ambao walimfichua mtu bubu mwenye pepo kwa kumpeleka kwa BWANA,
BWANA akamponya,
naye huyo bubu akanena kwa mara ya kwanza ,kisha makutano wakastaajabu.
Maana haikuwahi kuonekana katika Israeli wakati wote
(Mathayo 9 :32-33)

Kumbuka;

Yule bubu asin’geponywa kama asing’epelekwa kwa BWANA.
Watu walipoona yafaa kumpeleka,Wakampeleka mbele za Bwana,Naye akapokea uponyaji saa ile ile.

Nasi yatupasa kuwaleta wenye mapepo,magonjwa,wadhaifu,N.K
Wote hawa hawawezi kumwendea BWANA wao kama wao,muda mwingine yatupasa KUWAPELEKA ndipo waponywe.

Ili umpeleke mgonjwa kwa Bwana,Hakikisha kwanza wewe mwenyewe sio mgonjwa. Yaani uwe safi,
safi katika kila eneo,
uwe safi hata katika kinywa,
maana mgonjwa anahitaji maneno ya faraja
Kwa kumuambia mfano;

'' Utapona tu,yupo Yesu wa Nazareti asiyeshindwa na ilo tatizo lako.,…Polee mpendwa,hayo ni ya kawaida kabisa,mpe maisha BWANA Yeye atakutua mzigo wako…N.K ''

-Lakini sio uwe na maneno ya kumvunja moyo.

Haleluya…

Tuwapeleke wagonjwa kwa BWANA ambaye Yeye ni JIBU na mtatuaji wa kila aina ya shida.

Tuangalie mfano mwingine mmoja katika siku ya leo kwa habari ya KUJISALIMISHA KWA BWANA.
Nimekuambia kwamba,hiyo ndio njia ya kwanza ya kupokea uponyaji wako,
Na hapa tunasoma,

Marko 5:27-28,&34
'' aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.
34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.’’

Haleluya…

Huyu ni mwanamke aliyetokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, Alafu sio tu kutoka damu,sikia, Biblia inasema aliteswa sana kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.

*Oooh,Jesus,I’ve mercy on us…
Unajua watu wengi wakisoma maandiko kama haya yenye kuelezea shida za watu kama hizi,wanafikiri kwamba ilikuwa rahisi….

Mimi nasema hapana,
Haya mazingira tunayoyasoma katika maandiko matakatifu ni mazingira magumu sana,
Tazama habari hiyo hapo juu ya huyo mwanamke aliyetokwa na damu muda mlefu namna hiyo pasipo kupona na pia alipoteza mali zake zote,nasema alipoteza mali zake zotee,sio mali kidogo bali ni mali zake zote zilipotea,
na hata hapo bado hakukumfaa kitu.

Sasa utaona ni jinsi gani alivyokuwa akiteseka huyu mwanamke.
Lakini leo anatuambia habari njema maana haumwi tena,
Hateseki tena,
Hana msiba tena,
Maana amemwendea mmoja mwenye majibu juu ya tatizo lake la kutokwa damu.
Ni Yesu pekee ambaye ndie daktari wa kweli,
Yeye ni bingwa wa mabingwa.

Nalikuambia tunajifunza njia moja tu ya kupokea muujiza/uponyaji wako na ni
KUJISALIMISHA KWA BWANA.

Mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu muda mlefu huo,Yeye alipoijua siri hii ya uponyaji,
kwamba uponyaji halisi upo mbele za BWANA,alifunga safari na kumuendea mahali alipo BWANA.
Biblia inasema
'' aliposikia habari za Yesu,
alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;’’ Marko 5 :27

Sikia sasa,
Huyu mwanamke alikuwa ana akili nyingi sana,
Maana yeye alihitaji kwanza KUSIKIA HABARI ZA YESU.Kisha aliposikia AKACHUKUA HATUA kwa kupita kwa nyuma ya mkutano na kuligusa vazi lake.

Tazama hapo kwa makini Biblia inasema '' Aliposikia…'' IMANI ya mwanamke huyu ilianzia hapo kwa kusikia habari za Yesu Kristo.
Na mara tu baada ya kusikia AKAPIGA HATUA,
Hii ikimaanisha kwamba ALIPOKUWA NA IMANI AKAJUMLISHA NA MATENDO ya kugusa pindo la vazi la BWANA. Naye akapona na ule msiba saa ile ile.

Hizo hatua alizozichukua mwanamke huyu,ndizo hatua tutakazojifunza katika fundisho lijalo…

ITAENDELEA…
• Usikose fundisho lijalo mahali hapa,ambapo tutachimba zaidi.
Kwa maombezi;

• +255 767 674 089

COMPUTEC TRAINING COMPUTER WANAKULETEA COURSE ZA COMPUTER NYOTE MNAKARIBISHWA


Are you looking for?

computer  pragrames join computec training computer courses

computec it is located Kibaha kwamatias kibondeni karibu na kibao cha kanisa katoliki or  call me on +255 767 674 089 or email:hezzodaking@gmail.com


Mtumishi Cosmas Chidumle akihubiri


Mtumishi Cosmas Chidumle akihubiri

Kama ilivyo katika mkutano mwisho alisimama Gwiji la Mziki(Mwana Mziki halisi) ambae kwa sasa anamtangaza Yesu kwa Nguvu zake Mwinjilisti Cosmas Chidumle. Aliwaambia wakazi wa Vijibweni kuwa Kama ni Uhuni yeye alikuwa Mhuni zaidi, kama ni usharobaro basi alikuwa hivyo ila wa enzi hizo. Pamoja na maisha ya kujulikana aliyoyaishi kipindi hicho hakuwa na furaha kwani alikuwa amepungukiwa kitu. Yesu alipoingia katika maisha yake maisha yake yamekuwa ya tofauti sana. Mwinjilisti huyo aliutumia dakika kumi kuhubiri kutokana na kuchelewa kufika lakini hio ilikuwa Ijumaa lakini Jumamos Mungu anaenda kutembea kwa njia ya ajabu ambapo Mtumishi atasimama mapema na watu kwenda kufunguliwa.

Katika mkutano huo watu walimkubali Bwana Yesu na kuongozwa sala ya toba.

MKUTANO HUU UNALETWA NA KANISA LA T.A.G.

UKRISTO/UISLAM

HEZRON MARWA MWANAFUNZI WA YESU

          UKRISTO


Wakristo tunaamini kwamba Yesu ni mwana wa Mungu, aliteswa, alikufa na siku ya tatu alifufuka na pia tunaamini ndiye njia ya kutufikisha mbinguni na alipopaa kwenda mbinguni aliahidi kuleta msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu!

                   UISLAM



Ndugu Waislamu huamini ALLAH ndio Mungu, Yesu sio mwana wa Mungu,  alikuwa mmoja wa mitume wakubwa, alifanya miujiza  lakini hakufa msalabani ni““Hawakumuua wala hawakumsulubisha lakini walidhani wamefanya hivyo (Quran 4:156) “Mungu alimuinua …….(Quran 4:157).
—–KWA WALE WANAOTAKA KUJUA UKWELI KARIBUNI— MAWASILIANO +255 767 674 089

MAOMBEZI KWA JINA LA YESU YAKIFANYIKA NA WATU KUFUNGULIWA KUTOKA NGUVU ZOTE ZA GIZA ZILIZOKUWA ZIMEWAFUNGA

    ASKOFU SPEAR MWAIPOPO AKIOMBEA WAAMINI WOTE WA KANISA LA TAG PICHA YA NDEGE SHALOM TEMPLE, NA NGUVU ZOTE ZA GIZA ZILIZOKUWA ZIMEWAFUNGA KUTOWEKA KATIKA JINA LA YESU KRISTO
 

Kwanini nguvu za kanisa la kwanza hazionekani katika kanisa la leo?

Kwanini nguvu za kanisa la kwanza
 hazionekani katika kanisa la leo?
Naianza mada mpya kwa swali gumu na linaloweza kuibua mijadala mingi huko tuendako; lakini ambayo itakuwa ni changamoto historia ya kanisa sanjari na madhehebu ya Kikristo yaliyopo ulimwenguni kwa sasa. Kwa wasomaji wangu wa miaka mingi, mtakumbuka huko nyuma, niliwahi kuandika makala yenye kuchambua tofauti zilizopo kati ya “madhehebu ya Kikristo” na “Ukristo halisi”. Ninalazimika kurudi katika uchambuzi wenye mwelekeo huo; lakini lengo kamili likiwa ni kudhihirisha kimaandiko na kihistoria kuhusu kitendawili cha miaka mingi kuhusu tofauti kubwa iliyopo kati ya nguvu za kanisa la kwanza na udhaifu wa kanisa la leo. Najua kuna utetezi ambao umekuwa ukitolewa na kurasimishwa kama ndio sababu kamili. Lakini matukio ambayo yamejitokeza katika karne za hivi karibuni yanaufanya utetezi uliokuwepo kupoteza ushawishi; na hivyo kutoa mwanya wa kufanya upya utafiti wa kimaandiko na kihistoria; ili kupata majibu sahihi ambayo hayatapingika hata kama yasiyopokubaliwa kwa haraka. Katika kujenga msingi thabiti wa mada hii, nitaanza kwa muhtasari kuchambua kwanza tofauti kati ya “Ukristo” na “Madhehebu ya Kikristo”:
Tafsiri ya misamiati ya “Ukristo”
na “Madhehebu ya Kikristo”
Kwa msomaji mpya unaweza kudhani ninataka kukuchanganya kwa kusema kuna tofauti ya Ukristo halisi na Madhehebu ya Kikristo. Pengine wewe unafikiri vyote ni kitu kile kile, chenye maana moja, ila majina tu ndiyo yanatofautiana. Tusisahu pia kwamba tofauti za maneno zinatosha kuleta maana tofauti ya maneno husika. Nivumilie tu nijieleze ili unielewe na kujua kule ninakoelekea.
Tafsiri ya awali nainukuu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu, ili kupata maana ya maneno mawili ambayo, ni “Ukristo” na la pili “Madhehebu”. Maana za maneno haya zitatupa picha ya tofauti zilizopo kisha tunaendelea na uchambuzi kutoka vyanzo vingine vya lugha.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu imelitafsiri neno “Ukristo” kuwa ni: “Dini inayoamini kuwa Mungu ni mmoja, inayofuata mafundisho ya Yesu Kristo.”
Hapa neno Ukristo limetafrisiwa kuwa ni dini. Hapa inaonesha kwamba Ukristo umejumuishwa na dini nyingine kama vile Uislamu na Ubudha.
Tunapokuja kwenye msamiati wa neno “Madhehebu” tunakuta Kamusi ya Kiswahili Sanifu imelitafsiri katika maana tatu zifuatazo: 1. Fikira na mwongozo wa kidini unaotokana na uelewaji wake wa misingi ya dini hiyo na unaoleta tofauti ndogondogo za mawazo lakini zisizovunja misingi ya dini hiyo. 2. Wafuasi wa mawazo ya kiongozi wa dini. 3. Mwenendo fulani wa kufanya au kuendesha mambo.
Tukichukua tafsiri ya kwanza na kuihusisha na msamiati wa madhehebu ya Kikristo inaweza kusomeka kama ifuatavyo: “Madhehebu ya Kikristo ni fikira au miongozo ya kidini inayotokana na uelewaji wake wa misingi ya dini ya Kikristo na inayoleta tofauti ndogondogo za mawazo lakini sizizovunja misingi ya dini hiyo ya Kikristo.”
Tukichukua tafsiri ya pili na kuihusisha na msamiati wa madhehebu ya Kikristo inaweza kusomeka kama ifuatavyo: “Wafuasi wa mawazo ya viongozi waasisi wa madhehebu katika dini ya Kikristo.”
Mpaka hapo, tukizichukua maana za maneno yaliyotajwa ya, “fikira”, “Mawazo” “Miongozo inayoleta tofauti ndogondogo za mawazo” tunaweza kufikia muafaka kwamba maana ya jumla ya Kiswahili kuhusu  madhehebu ya Kikristo inaweza kusomeka kama ifuatavyo: “Itikadi za kimakundi zilizoasisiwa na viongozi mbali mbali wa madhehebu ya Kikristo yanayotumia mwavuli wa dini ya Kikristo
Tukiishia katika maana iliyotokana na Kamusi ya Kiswahili Sanifu, tutakomea katika uelewa kwamba, madhehebu ya Kikristo na Ukristo ni kitu kimoja lakini chenye tofauti ndogondogo zinazotokana na mawazo ya viongozi wa makundi husika.
Je! Hii ndio maana yake halisi? Je! Tafsiri ya Kiswahili iliyopo imechukua maana sahihi ya maneno husika kutoka kwenye vyanzo sahihi vya lugha nyingine zilizotangulia kutumia maneno haya?
Kimsingi, tukitaka kujua maana sahihi ya neno, hususani lile lililoazimwa kutoka katika lugha nyingine, ni muhimu kurejea kwenye lugha asilia na kujifunza matumizi asilia ya neno hilo kabla halijahamishiwa katika lugha nyingine. Na hii ndiyo kazi nataka tuifanye hivi sasa katika uchambuzi wa maneno ya “Ukristo” na “Madhehebu ya Kikristo” jinsi yalivyotangulia kutumika kwenye lugha asilia kabla hayajahamishiwa katika Kiswahili chetu.
Chimbuko la msamiati ya “Ukristo”
Katika maandiko matakatifu ya Agano Jipya hakuna msamiati wa neno “Ukristo”. Kuna maneno mawili yafuatayo: 1. Kristo, na 2. Mkristo. Maana ya neno la kwanza la Kristo ni “Christos” likimaanisha “mpakwa mafuta”. Neno la pili la “Mkristo” kwa lugha asilia ni: “Christianos” likimaanisha “mfuasi wa Kristo”. Neno hili lilitajwa kwa mara ya kwanza mnamo karne ya pili ambapo watu wa mataifa waliamua kuwaita wenye kumwabudu Yesu kuwa ni “Wakristo
“hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.” (Mdo.11:26)
Mara ya pili tunakutana na msamiati wa neno “Mkristo” wakati Paulo alipokuwa akijitetea mbele ya kiongozi katika dola ya kirumi jina lake Agripa. Huyu alisikiliza utetezi wa kiimani wa Paulo akajikuta anashawishiwa kufanyika mfuasi wa Kristo mpaka akamwonya Paulo kwa maneno yafuatayo:
“Agripa akamwambia Paulo, kwa maneno machache wadhani kunifanya Mkristo.” (Mdo.26:28)
Mara ya tatu tunakutana na msamiati wa neno “Mkristo” wakati Petro alipokuwa akiwausia na kuwatia moyo wafuasi wa Kristo ili kila Mkristo atetee imani yake hata kama yu katika mateso isivyo halali:
“Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.” (1 Pet.4:16)
Kufuatia nukuu za maandiko kuhusu msamiati wa neno “Ukristo” tumebaini neno hili halijaandikwa kwenye nyaraka za Agano Jipya. Badala yake tumekutana na maneno ambayo yanafanana na huenda ndiyo yaliyosababisha kuzaliwa kwa msamiati wa neno “Ukristo”.
Hapa tunajifunza kwamba, msingi na chimbuko la “Wakristo” na “Mkristo” ni Yule mwenye jina hilo tangu mwanzo ambaye ni Yesu Kristo. Huko Antiokia, wanafunzi wa Yesu, badala ya kuendelea kuitwa kwa jina refu la wanafunzi wa Yesu Kristo” wakapewa jina fupi la ”Wakristo” lenye kuonesha moja kwa moja mahusiano yaliyopo ya kiimani kati yao na Kristo mwenyewe. Huko Baadaye neno “Mkristo” lilitumika kumtambulisha mwamini mmoja mmoja.
Katika historia ya mwanzo wa matumizi ya maneno haya “Wakristo” na “Mkristo” hatusomi habari za “mawazo” au “itikadi za kimakundi” katika imani ya Kikristo. Waliotajwa kutumia maneno haya hatusomi kwamba yalikuwa ni majina ya kimakundi au kiitikati zenye “tofauti ndogondogo” za mawazo ya waasisi wa kiimani. Ni maneno yaliyobadilika kuwa majina ya kundi lile lile moja, lenye imani moja, ubatizo mmoja, Bwana mmoja, ambalo lilikuwa likiongezeka idadi na kuenea katika miji na nchi mbali mbali za ulimwengu wa karne ya kwanza.
Kwa bahati mbaya, katika nyaraka za asili za Agano Jipya, hatuna msamiati wa neno, “madhehebu ya Kikristo” kwa maana ya tafsiri ile tuliyoipata kwenye Kiswahili chetu isemayo: “Itikadi za kimakundi zilizoasisiwa na viongozi mbali mbali wa madhehebu ya Kikristo yanayotumia mwavuli wa dini ya Kikristo
Kwa mantiki hii, kinachoweza kutusaidia kujua chimbuko la msamiati wa madhehebu ya Kikristo kwa maana ya “itikadi za kimakundi” katika imani ya Kikristo, si kingine bali ni historia ya kanisa, ambayo tunaendea kuipitia kwa ufupi kama ifuatavyo:
Chimbuko la “Madhehebu ya Kikristo”
Katika karne za kwanza za historia ya Ukristo, hakukuweko kabisa “madhehebu ya Kikristo” kama tuliyo nayo hivi leo. Japokuwa zilijitokeza changamoto za kuibuka kwa vijikundi vilivyokuwa vikijimega, vingi vilikuwa vidogo na wafuasi wake waliitwa “Wazushi” wala hawakuhesabiwa kuwa ni sehemu ya Ukristo. Tangu kipindi cha mwanzo wa Ukristo  kulikuwepo kanisa moja tu la “Katoliki” kwa maana ya “kanisa la ulimwengu mzima”. Kimsingi, mwamini yeyote ambaye hakuwa mshirika katika kanisa hilo hakutambuliwa kuwa ni Mkristo.
Historia ya “Madhehebu ya Kikristo” inaanza na kitu kinachoitwa “Mgawanyiko wa kanisa”. Mngawanyiko wa kwanza mkubwa ulijitokeza kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1054 uliotokana na “Great Schism” kati ya Kanisa la Mashariki na Kanisa la Magharibi. Kuanzia hapo kukawepo makundi makubwa mawili ya kikristo ambayo baadaye yalikuja kujulikana kama Kanisa Katoliki la Magharibi na kanisa la Mashariki la Orthodox
Mgawanyiko mkubwa wa pili wa kanisa ulitokea katika karne ya 16 wakati wa Matengenezo Kiprotestanti ambayo mwasisi wake alikuwa Martin Luther. Katika kuonesha kutokuridhishwa kwake na mwenendo wa imani ya Kanisa mnamo mwaka 1517 alichapisha na kubandika mambo 95 (Thesis) ambayo hatimaye mnamo mwaka 1529 yalianzisha rasmi vuguvugu la Uprotestanti.
Hoja ya msingi iliyoleta mgawanyiko ni madai ya uhuru wa kuyatafsiri mambo ya imani na wokovu wa Mungu kama jambo linalomhusu mtu binafsi na Mungu, pasipo kupitia kwa mtu au taratibu za kitaasisi zenye kusimamiwa na binadamu.
Katika kuweka mkazo wa jinsi hii, wa uhuru wa kila mtu kujitafsiria maandiko na kusimama mbele za Mungu kwa imani yake, kukaligawa kanisa na kuwa na makundi mawili ambayo ni “Uporotestanti” na “Ukatoliki”. Kundi la Ukatoliki likaendelea na msimamo wake kwamba wa tafsiri ya maandiko na mafundisho kuwa chini ya udhibiti wa utawala wa kanisa ili kuepusha kuwachanganya wafuasi kwa sababu ya kila mtu kujitafsiria mambo yake binafsi.
Kundi lililomeguka kutoka kwenye “Ukatoliki” lenyewe likaendeleza vuguvugu lake jipya la kupinga kwamba utaratibu wa kudhibiti tafsiri ya maandiko tayari kulikwisha kusababisha uharibifu wa imani ya kweli ya Ukristo. Likaendelea kusisitiza kwamba waamini wapewe uhuru wa kujisomea maandiko wenyewe na kuyatekeleza kwa jinsi wanavyoongozwa na dhamiri zao wenyewe.
Vuguvugu la matengenezo lilipoanza huko Ujerumani, ndipo makundi mengine katika sehemu za Ulaya nayo yakaanza kumeguka kutoka katika Kanisa Katoliki. Wakajitokeza wana-matengenezo kama Ulrich Zwingli na John Calvin na John Knox ambao waliasisi makundi ya kimethodist, Presbyterian, wabaptisti na kadhalika.

Kwanini nguvu za kanisa la kwanza hazionekani katika kanisa la leo?