Powered By Blogger

Jumanne, 6 Mei 2014

SAYUNI BAND IKO WAPI NJIA.

                        SUMBAWANGA MKUTANO WA INJILI.

MKUTANO MKUU WA INJILI SUMBAWANGA MJINI AMBAO UNAONGOZWA NA KANISA LA T.A.G. ULIO ANZA TAREHE 27/04/2014 MUHUBILI TOKA DAR ES SALAAM WAIMBAJI TOKA MBEYA SAYUN BAND NDIO WAHUDUMU WA MKUTANO HUO AMBAO UNAENDELEA MKOANI HUMO.

MUHUBILI HUYO AMEWAHASA WACHAWI KUA MDA HUU NDIO WAKUJISALIMISHA MANA YESU NDO ANAANZA OPERATION KABLA UJABAINIKA JISALIMISHE ALISEMA MCHUNGAJI HUYO.



MUHUBILI HUYO ALIZIDI KUSISITIZA WACHAWI WOTE HAWANA MAANA ZAIDI NI BORA WAJE KWA YESU ILI YEYE AWAPUMZISHE MANA KAZI YA KUPAA USIKU YESU KAISIMAMISHA NI MDA HUU WA KUMREJEA MUNGU WAO ALISEMA MCHUNGAJI HUYO     
MJINI SUMBAWANGA LEO.

Emmanuel Mgogog
 akiwa na kundi lake hapo mjini sumbawanga leo katika mkutano mkuu wa injili unaendelea mjin hapo kiongozi huyo Mgogo amesema wamemuona Mungu katika mkutano huo akifanya mambo yaajabu watu wakipokea uponyaji kwa njia ya uimbaji na pia watu wakibalikiwa mjini hapo sumbawanga Mgogo alisema.
Hapo ni umati wa watu wakiitikia wimbo wa kuabudu ulio imbwa na Emmanuel Mgogo mjin hapo.


 Hapo tunawaona waimbaji wa Sayuni Band wakiongozwa na Emmanuel Mgogo baada ya mkutano unaoendelea mkoani hapo.kutoka kulia ni Neema,katikati tunamwomwona kinala wa sauti ya kwanza katika band hiyo Victoria akifatiwa na Rusy Saimon.
 Hapo tunamwona kiongozi wa sayuni Band Emmanuel Mgogo akifatilia mahubili kwa umakini mnooo.
Hapo ndipo watu wakinyosha mikono yao juu na kusalenda mbere ya Yesu Kristo wakisema Mungu hawalehemu na kuwabaliki kwa maandalizi ya kesho ya mkutano huo unaoendelea mkoani hapo.

Sayun Band wamiliki wa blog hiii ukitaka kuwasiliana nao au kufanya huduma nao mahari popote maeneo yeyote utawapata kwa mawasiliano hayo hapo chini.
+255 718 89 82 70

WAIONAYO NJIA YA UZIMA NI WACHACHE SANA.



Njia iendayo katika mateso ya moto ni pana sana na waingiao ni wengi sana.Si wote waimbao kwaya,kushika biblia n.k waendao mbinguni.Mathayo 7:21 

wengi wenye majina makubwa makubwa hata wengine ni wachungaji,mapadre mashehe, maraisi, mawaziri n.k watakwenda njia ile pana.

Ni wachache sana waendao mbinguni.Hatupaswi kuridhika tu kuhudhuria ibada kama hii kwani hata shetani anaingia kwenye nyumba za ibada Ayubu 1:6 .

Si swala la kumwabudu MUNGU mmoja kwani pia mashetani hufanya hayohayo tena kwa kutetemeka.Yakobo 2:19.

Moto wa milele uliubwa kwa ajili ya shetani na malaika zake na MUNGU hakukusudia kabisa kumwachilia mwanadamu aende huko.Lakini wengi wanakwenda huko kwa kukosa maarifa ama kufuata tu mkumbo.Mtu anakuja kanisani kwa lengo tu Fulani mfano kuwafuata wazazi kutafuta misaada ama fedha,wachumba ,kazi ,chakula n.k na ukimpima katika mizani ya utakatifu utakuta hayupo yupo duniani kabisa.

Lazima tufahamu kuwa kuna maisha baada ya hapa duniani na hatutaishi hapa duniani milele na milele.Hapa sisi wote ni wasafiri na wapitaji.Mathayo 25:41.Tuwe macho tusije tukaaibika kama wale wasio na matumaini.Tusifuate tu mkumbo jiulize endapo kweli umeokoka.

BWANA YESU pekee ndiye anayeokoa(Yohana 14:6)

Soma kwa makini kisha ''Share'' kwa marafiki zako kwani utawaponya wengi ili wampe YESU maisha yao na kuokolewa.

MUNGU akubariki sana.

Jumatatu, 5 Mei 2014

HEZRON MARWA MWANAFUNZI WA YESU
Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...

Siku ya leo,Bwana Mungu akuhudumie kwa namna ya tofauti tunapomalizia hii tafakari.

Kumbuka, tulikuwa tumekwamia kuchimba kiundani katika tafakari,

Tukijifunza juu ya njia moja ya kwanza ya kupokea muujiza/jibu lako kutoka kwa mwenye majibu ambaye ndie wa milele,

Ni Bwana wa mabwana,
Mfalme wa wafalme,
Mungu mwenyezi,
JEHOVA aliyekuwepo,aliyepo na atakayekuwapo milele na milele.

Tulijifunza njia moja ya kupokea jibu lako nayo hiyo njia nilikuamba ni kujisalimisha kwake BWANA.

Leo tunajifunza njia nyingine ya kupokea jibu lako.
Kumbuka kwamba,
Kila jibu juu ya swali ulilonalo lipo kwa BWANA.

Labda kabla hatujaangalia njia nyingine itupasayo kupokea majibu kutoka kwa Bwana,
Niseme hivi;

Katika njia hiyo ya kujisalimisha kwa Bwana,ipo gharama ikupasayo kuilipa.

Gharama yenyewe ni ya kuidharau aibu.

Aibu ni gharama,
Aibu hutesa maisha yetu,
Wengi,hatupokei kwa sababu ya kuwa na AIBU.

Mungu leo atusaidie sana tuweze kuidharau aibu.

Ili ujifichue na umfuate Bwana Yesu,lazima ukubali kuacha yote.

Tazama sasa;
jamii inayokuzunguka itakusema vibaya,kwa sababu ya kumfuata Bwana Yesu.

Kujisalimisha kwa Bwana Yesu ni kuokoka.

*kuokoka ni kukutana na Yesu.

TAMASHA kubwa la kwanza la kusifu na kuabudu lilofanyika pale Dar es salaam


Ijumaa, 2 Mei 2014

Makamu wa Askofu asisitiza Katiba bora

MAKAMU wa Askofu Jimbo la Mashariki Kaskazini, Mchungaji Spear Mwaipopo, amesema Kanisa litaendelea kuliombea Taifa na viongozi wake, lakini akawataka viongozi wa nchi hii nao watimize wajibu wao kwa kutenda haki.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam katika ibada ya kuadhimisha miaka 75 ya Kanisa hilo nchini.

Mchungaji Mwaipopo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alisema; "Kama kanisa tutaendelea kuliombea Taifa, lakini na Viongozi wa nchi hawana budi kutimiza wajibu wao wa kulitendea haki Taifa letu kwa kudumisha Muungano, amani na mshikamano na kutupatia Katiba bora inayotokana na maoni ya wananchi."

"Sasa hivi kuna mabishano ya kiitikadi yanayoendelea na sisi tusingependa kuwa na Katiba ya Chama bali ya Watanzania wote... hakuna chama chenye watu zaidi ya milioni 45. Tukiruhusu hali hii tutakuwa hatuwatendei haki Watanzania walio wengi," alisema.

Alisema kila jambo jema hushuka kutoka kwa Baba wa mianga na kwamba kama Kanisa wamekuwa wakiliombea jambo hilo, hivyo anaamini kwamba Mungu atalisimamia hadi mwisho.

Aliwataka waumini wa Kanisa hilo kuendelea kuomba bila kuchoka. "Kwa hiyo wapendwa msiangalie malumbano tu ndani ya TV, bali endeleeni kuomba ili jambo hili aliloliazimia Bw. Liweze kutimia," alisema.

Alisema anafurahishwa na ukweli kwamba Kanisa la TAG linaadhimisha miaka 75 wakati Taifa la Tanzania limetimiza miaka 50 hapo jana tu (Aprili 26, 2014).

"Nawapongeza Marais wetu wastaafu hayati Mwl. Nyerere na Abeid Amani Karume kwa kudumisha Muungano wetu na kuruhusu kikatiba uhuru wa wananchi kuabudu. Kudumu kwa Muungano kumetusaidia kuweza kuhubiri Injili hadi Zanzibar," alisema.

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG-Taifa) lilianzishwa mwaka 1939 na kanisa la kwanza hapa nchini lilijengwa katika kijiji cha Igale, mkoani Mbeya.